London, England
Bao la dakika ya 90 lililofungwa na Conor Gallagher leo limeiwezesha Chelsea kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace huo ukiwa ushindi wa kwanza kwa kocha mpya wa timu hiyo, Graham Potter kwenye Ligi Kuu England akiwa na timu hiyo.
Kabla ya bao hilo pia ilikuwa nafasi nyingine ya mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Pierre-Emerick Aubameyang naye kuifungia timu hiyo bao la kwanza katika ligi hiyo alipoujaza mpira wavuni dakika ya 38 akiitumia pasi ya kichwa ya Thiago Silva na kusawazisha bao la Palace lililofungwa na Odsonne Edouard kaika dakika ya saba.
Aubameyang ambaye alikuwa akiichezea Arsenal lakini mwanzoni mwa mwaka huu alitimkia Barcelona baada ya kutokuwa na maelewano mazuri na kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, hatimaye mchezaji huyo alirudi England na kujiunga na Chelsea akiwa miongoni mwa usajili wa mwisho mwisho wa klabu hiyo katika majira ya kiangazi hivi karibuni.
Matokeo hayo yanaifanya Chelsea ikiwa nafasi ya tano kuwa nyuma ya vinara wa ligi hiyo, Arsenal kwa tofauti ya pointi nane ingawa ni matokeo ya kujivunia kwa Potter tangu achukue mikoba ya kuinoa timu hiyo akimrithi Thomas Tuchel aliyetimuliwa kutokana na matokeo mabaya.
Nayo Liverpool bado mambo yake si mazuri baada ya kupata sare ya mabao 3-3 ikiwa nyumbani dhidi ya Brighton wakati vinara Arsenal wameendelea vyema na kasi yao baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya mahasimu wao wa London, Tottenham.
Matokeo ya ligi hiyo mechi za leo ni kama ifuatavyo…
Arsenal 3-1 Tottenham
Bournemouth 0-0 Brentford
Crystal Palace 1-2 Chelsea
Fulham 1-4 Newcastle
Liverpool 3-3 Brighton
Southampton 1-2 Everton
West Ham 2-0 Wolves
Soka Potter aanza na ushindi Chelsea
Potter aanza na ushindi Chelsea
Related posts
Read also