London, England
Baada ya kufungwa mabao 3-1 na Arsenal, kocha wa Tottenham, Antonio Conte ameponda viwango vya waamuzi wa Ligi Kuu England (EPL) akitaka waamuzi hao wawe na tabia ya kukutana mara kwa mara.
Katika mechi hiyo maarufu London Derby iliyopigwa leo kwenye Uwanja wa Emirates, Arsenal walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Thomas Partey kabla ya Harry Kane kusawazisha kwa penalti na baadaye Arsenal kuongeza mabao mawili yaliyofungwa na Gabriel Jesus na Granit Xhaka.
Tottenham ilipata pigo baada ya mchezaji wake, Emerson Royal kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa rafu aliyomchezea Gabriel Martinnelli, uamuzi ambao Conte alisema uliua mchezo kwa upande wao kabla ya baadaye kulaumu waamuzi kwa ujumla. Wakati Emerson anatolewa, Arsenal walikuwa wakiongoza kwa mabao 2-1.
“Kuna wakati unakuwa mwenye bahati, kuna wakati huna bahati, kadi nyekundu iliua mchezo, huu ni ukweli lakini si kwa sababu tulibaki 10 , ni kwa sababu timu yetu ilikuwa ikiwaandama zaidi na zaidi na hata katika dakika nne au tano za kufanya mabadiliko tukawa tunawaandama kiasi kwamba ikawa vigumu kwetu kujilinda na hapo tukafungwa bao la tatu.
“Kuna wakati unaona mazingira ya kadi ya njano lakini badala yake inatolewa nyekundu, wanatakiwa kulifanyia kazi jambo hili, nchini Italia kwa mfano waamuzi wetu wanakutana pamoja Alhamisi kwa siku tatu ili kufanya kazi pamoja, wanaangalia video ili kuboresha utendaji kazi wao,” alisema Conte.
“Sijui kama hili linafanyika England lakini litakuwa wazo zuri kwa sababu kiwango cha uchezaji kipo juu sana, tunahitaji kuwa na kiwango cha waamuzi waendane na VAR, unaelewa kwa sababu Ligi Kuu ipo juu mno, kwa maoni yangu kila eneo linalohusisha ligi hii lazima liwe katika kiwango cha juu.
“Nalazimika kuwa mkweli, kuna ugumu mno kwa sababu hawana msimamo mmoja, unanielewa, kuna wakati unaiona hali ambayo kadi nyekundu inatakiwa kutolewa badala yake inatolewa ya njano au haitolewi hata hiyo ya njano,” alisema.
Kimataifa Conte ahoji uwezo wa waamuzi EPL
Conte ahoji uwezo wa waamuzi EPL
Related posts
Read also