Tiraspol, Moldova
Kocha wa Man Utd, Erik ten Hag amempongeza Cristiano Ronaldo na kuongeza kwamba mchezaji huyo alihitaji kupata bao baada ya kufunga bao lake la kwanza msimu huu katika mechi ya Europa Ligi dhidi ya Sheriff Tiraspol, Alhamisi usiku.
Ronaldo alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penalti dakika ya 39 katika ushindi wa mabao 2-0 mjini Tiraspol na kuifanya Man United kupata pointi tatu muhimu katika Europa Ligi. Kwa Ronaldo hilo ni bao lake la kwanza katika mechi zake nane za msimu huu.
“Ronaldo alihitaji kufunga goli lile, amekuwa mara nyingi akikaribia kufunga lakini hicho ndicho alichokuwa akikitaka sana, tunamfurahia na timu inamtaka afunge, unajua kwamba Cristiano atafunga tu kwenye penalti,” alisema Ten Hag akizungumzia bao hilo ambalo lilikuja baada ya Jadon Sancho kuipatia timu hiyo bao la kwanza dakika ya 17.
Ten Hag pia alimpongeza Sancho akisema kwamba tayari mchezaji huyo ana mabao mengi katika mechi za maandalizi ya msimu, “Anaendelea vizuri ingawa nafikiri bado kuna nafasi ya kuwa bora zaidi kwa sababu ana mbinu nyingi, unapoma nafasi akiwa uwanjani na anapojiamini anaweza kuwa bora zaidi.”
Matokeo ya Europa Ligi ni kama ifuatavyo…
Bodo 2-1 Zurich
Dynamo Kyiv 0-1 AEK Larnaca
Rennes 2-2 Fenerbahçe
Real Betis 3-2 Ludogorets Razgrad
Roma 3-0 HJK Helsinki
Sporting Braga 1-0 Union Berlin
Union Saint-Gilloise 3-2 Malmö FF
Real Sociedad 2-1 Omonia Nicosia
Sheriff Tiraspol 0-2 Man United
FC Midtjylland 5-1 Lazio
Feyenoord 6-0 SK Sturm Graz
FK Qarabag 3-0 Nantes
Olympiakos 0-3 SC Freiburg
Monaco 0-1 Ferencvárosi TC
Trabzonspor 2-1 Red Star Belgrade
Kimataifa Hatimaye Ronaldo atupia, Ten Hag ampongeza
Hatimaye Ronaldo atupia, Ten Hag ampongeza
Related posts
Read also