Manchester, England
Sasa ni rasmi winga Antony hatimaye amemwaga wino kuichezea klabu ya Manchester United akitokea klabu ya Ajax ya Uholanzi kwa ada ya Pauni 82 milioni.
Antony mwenye umri wa miaka 22, amewahi kufanya kazi na kocha wa sasa wa Man Utd, Erik ten Hag wakati huo kocha huyo akiinoa Ajax ambapo katika mkataba wake wa miaka mitano kuna kipengele ambacho kinaipa nafasi klabu hiyo kuongeza mwaka mmoja.
Akizungumzia kukamilika kwa usajili huo, Antony alisema,”Hili ni jambo kubwa katika maisha yangu ya soka, kujiunga na moja ya klabu kongwe duniani, namshukuru kila aliyeniamini hususan familia yangu, makocha wangu na wachezaji wenzangu kwa sababu nisingeweza kufika hapa bila ya wao.”
“Kucheza chini ya Erik ten Hag katika klabu ya Ajax lilikuwa jambo sahihi kwangu na maendeleo yangu, aina ya soka lake na ufundishaji wake vinanifanya kuwa bora, na nina furaha kwa kile alichoniambia kuhusu mipango na matamanio yake Manchester,” alisema.
Antony amefunga mabao saba ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika mechi 11 za michuano hiyo akiwa na Ajax na ameifungia timu ya Taifa ya Brazil mabao mawili katika mechi tisa alizoichezea timu hiyo tangu Oktoba 2021 alipoitwa mara ya kwanza.
Mbali na Antony, Man Utd pia imemsajili kipa wa Newcastle, Martin Dubravka kwa mkopo huku kukiwa na makubaliano ya kumsajili moja kwa moja kwa ada ya Pauni 6 milioni kama atapata nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza.
Kipa huyo kutoka Slovakia amecheza mechi zaidi ya 125 za Ligi Kuu England katika misimu mitano na ameichezea timu yake ya Taifa ya Brazil mara 29.
Kimataifa Antony rasmi mali ya Man Utd
Antony rasmi mali ya Man Utd
Related posts
Read also