Na mwandishi wetu
Jumapili haikuwa nzuri kwa Taifa Stars baada ya kushindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani wa Benjamin Mkapa kwa kufungwa bao 1-0 na Uganda Cranes katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).
Stars ililala kwa bao la dakika ya 87 lililofungwa na Travis Muytaba na hivyo kuiweka katika wakati mgumu timu hiyo kwani sasa itakuwa na kazi ya kuhakikisha inapata ushindi wa ugenini katika mechi ya marudiano wikiendi ijayo ni jambo gumu lakini dakika 90 zinaweza kuja na matokeo yanayoweza kuwafurahisha Watanzania, tusubiri.
Stars ilianza kwa kuitoa Somalia kwa jumla ya mabao 3-1, ilianza kwa ushindi wa bao 1-0 na kufuatiwa na ushindi mwingine wa mabao 2-1 katika mechi ambazo zote zilipigwa kwenye Uwanja wa Mkapa kutokana na hofu ya usalama iliyopo nchini Somalia.
Michuano ya CHAN ilizinduliwa rasmi mwaka 2009 na kufanyika nchini Ivory Coast kwa mara ya kwanza ambako Tanzania ilifuzu lakini iliishia katika hatua za awali wakati huo ikinolewa na kocha kutoka Brazil, Marcio Maximo.
Kimataifa Stars yajiweka pagumu CHAN
Stars yajiweka pagumu CHAN
Read also
