Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Geita Gold, Fred Felix Minziro amesema kwamba anaamini wiki mbili za mapumziko ya Ligi Kuu ya NBC zinamtosha kurekebisha kasoro nyingi zilizoonekana katika kikosi hicho kwenye mechi mbili walizocheza.
Geita inayoshika nafasi ya 13 imefungwa mechi ya kwanza na Simba mabao 3-0 kisha ikatoa sare ya 1-1 na Azam. Mechi zote Geita ilikuwa ugenini.
Minziro ameeleza kuwa hajafurahishwa na mwenendo walioanza nao ikizingatiwa kuwa msimu uliopita walimaliza kwenye nafasi ya nne na kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.
Alifafanua kuwa hayo yametokea kwa sababu nyingi lakini mojawapo ni kukosa maandalizi ya maana wakati wakijiandaa na msimu mpya wa ligi, lakini akaahidi kuyashughulikia mapungufu hayo kikamilifu ndani ya wiki mbili hizi.
“Ni kweli tumeanza vibaya hatukuwa vizuri, naweza kusema ni sababu ya kukosa maandalizi sahihi wakati tunajiandaa na msimu huu lakini nimeona makosa, mapungufu, shida iko wapi na ninaamini wiki mbili hizi tulizonazo zinanitosha kuweka mambo sawa.
“Ligi si nyepesi, kila mmoja amejiandaa na si kwamba tuna timu inayoshindwa kupambana isipokuwa ni kujiweka fiti zaidi na kurekebisha matatizo tuliyonayo, tutarudi kwenye ubora wetu unaofahamika,” alisema Minziro.
Ligi ikirejea, Geita itakuwa nyumbani kuumana na Kagera Sugar Agosti 6 kabla ya mchezo wao wa hatua ya awali wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Hilal Alsahil ya Sudan ambao utachezwa Agosti 9 mwaka huu.
Soka Minziro kutumia wiki 2 kurekebisha kasoro Geita
Minziro kutumia wiki 2 kurekebisha kasoro Geita
Related posts
Read also