Na mwandishi wetu
Aliyekuwa kocha wa Polisi Tanzania msimu uliopita, Malale Hamsini amefunguka kushindwana na timu alizokuwa anazungumza nazo kwa ajili ya kuzinoa msimu huu hivyo ameamua kupumzika.
Malale aliachana na Polisi baada ya kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu ya NBC 2021/22 akiiongoza timu hiyo kwenye mechi 30, ikimaliza kwenye nafasi ya nane kwa pointi 37 na mikoba yake kupewa Joslin Shariff raia wa Burundi.
Ilielezwa hata hivyo kuwa kocha huyo yupo kwenye mazungumzo ya kujiunga na miongoni mwa timu zinazoshiriki Ligi ya Champioship lakini baadaye wakashindwana.
Akizungumza na GreenSports, Malale alisema alikuwa kwenye mazungumzo na timu takriban tatu lakini zote wamemaliza mazungumzo yao bila kuafikiana na sasa ameamua kupumzika akisubiri ngwe nyingine ya mazungumzo na timu nyingine zitakazomhitaji.
“Ilikuwa nijiunge na timu moja hivi karibuni lakini imeshindikana, zilikuwa kama tatu lakini ikabaki hiyo moja na sasa nipo tu nimepumzika kwanza labda tuangalie kwa ngwe nyingine na kama nitajiunga na timu yoyote basi mapema tu itawekwa wazi,” alisema Malale kocha wa zamani wa Ruvu Shooting na Alliance FC.
Soka Malale Hamsini aamua kupumzika
Malale Hamsini aamua kupumzika
Related posts
Read also