London, England
Kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel anachunguzwa na FA kwa kauli aliyoitoa dhidi ya mwamuzi Anthony Taylor aliyechezesha mechi ya Chelsea na Tottenham Jumapili kwenye dimba la Stamford Bridge na timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2.
Tuchel anadaiwa kusema, “Labda Taylor asiwe mwenye kuchezesha mechi zinazowahusisha Chelsea siku zijazo.” Tuchel alitoa kauli hiyo kuelezea hasira alizokuwa nazo kutokana na mabao mawili ya Tottenham katika mechi hiyo.
Katika mechi hiyo, Chelsea walikuwa mbele kwa bao 1-0 kabla Tottenham hawajasawazisha kupitia kwa Pierre-Emile Hojbjerg, bao ambalo hapo kabla ilionekana kama Rodrigo Bentancur alimchezea rafu Kai Havertz lakini mwamuzi hakufanya lolote.
Dakika 13 zikiwa zimebaki kabla ya mpira kumalizika, Reece James aliipatia Chelsea bao la pili lakini katika dakika za nyongeza Cristian Romero hakupewa adhabu licha ya kumvuta nywele Marc Cucurella wakati wachezaji hao wakipambana wakiwa kwenye kona.
Katika dakika hizo hizo za nyongeza, Harry Kane aliipatia Tottenham bao la pili akiutumia mpira wa kona uliopigwa na Ivan Perisic na kuzifanya timu hizo zigawane pointi.
Mabao ya Tottenham yaliwazulia balaa makocha Tuchel na Antonio Conte wa Tottenham ambao wote walijikuta wakipewa kadi nyekundu na hivyo kila mmoja wa atatumikia adhabu ya kukosa mechi moja kwenye benchi la timu yake.
Tuchel alishutumu namna Taylor alivyochezesha mechi hiyo kwa kusema, “Sielewi ni kwanini bao la kwanza si la kuotea na sielewi inakuaje mchezaji anapomvuta mwenzake nywele na mchezaji aliyefanya hivyo anabaki uwanjani.”
Kimataifa Tuchel aingia matatani
Tuchel aingia matatani
Read also