Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo amesema yupo tayari kwa mapambano ya kuwania nafasi ya kucheza bila kujali upinzani uliopo ndani ya kikosi hicho.
Awali, ilielezwa kuwa Makambo yumo kwenye orodha ya wachezaji waliotakiwa kutemwa kwenye timu hiyo kutokana na kiwango cha chini alichokionesha msimu uliopita lakini uongozi na benchi la ufundi ukaamua kumpa nafasi nyingine.
Mshambuliaji huyo raia wa DR Congo ameeleza kuwa mipango yake kwa msimu ujao ni kupambania nafasi ya kucheza na siyo kukaa benchi, lengo lake ni kuthibitisha uwezo wake halisi kwa benchi la ufundi linaloongozwa na Nasreddine Nabi raia wa Tunisia.
“Ni kweli msimu uliopita haukuwa mzuri sana kwangu, sababu sikutimiza vyema majukumu yangu, lakini kwa msimu ujao sitokubali kukaa benchi ndiyo manaa nipo mazoezini tangu siku ya kwanza timu ilivyoanza kambi lengo ni kucheza na siyo kukaa benchi,” alisema Makambo.
Mshambuliaji huyo mwenye rekodi ya kuifungia timu hiyo mabao 17, kwenye msimu wake wa kwanza kuitumikia timu hiyo kabla ya kuuzwa nchini Guinea, ameeleza kuwa anajua ushindani wa namba umeongezeka kwenye nafasi hiyo lakini hilo halimtishi hata kidogo.
“Cha msingi ni kupambana uwanjani, mazoezini ili kumshawishi kocha, hakuna kingine na ninaamini kwa juhudi nilizonazo na Mungu akinijaalia nitafanya vizuri msimu ujao,” alisema Makambo.
Nafasi ya Makambo kwa sasa inaonekana kuzidi kuwa finyu baada ya ujio wa washambuliaji Bernard Morrison, Aziz Ki na Lazarous Kambole huku tangu awali akiwa anachuana na Fiston Mayele ambaye ndiye mfungaji bora wa timu hiyo msimu uliopita.
Soka Makambo apania kupigania namba Yanga
Makambo apania kupigania namba Yanga
Related posts
Read also
