Na mwandishi wetu
Jumla ya wachezaji watano wa Azam wameungana na timu hiyo iliyoweka kambi yake nchini Misri na kukamilisha idadi kamili ya kikosi hicho kujiandaa na michuano ya msimu ujao 2022/23.
Wachezaji hao waliojiunga na Azam yenye wiki mbili sasa tangu itue nchini humo ni Abdul Sopu, Lusajo Mwaikenda na Pascal Msindo waliokuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa, Taifa Stars inayowania kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).
Wengine ni Mzambia, Rogers Kola na Mghana, Daniel Amoah ambao hawakujiunga na timu hiyo kutokana na ruhusa maalum waliyopewa.
Wachezaji hao tayari wameanza mazoezi leo asubuhi kwa ajili ya kumalizia ngwe ya mwisho ya maandalizi hayo wakitarajia kurejea nchini Agosti 12, tayari kwa Ligi Kuu Bara itakayoanza kuunguruma Agosti 15 mwaka huu, huku mechi yao ya kwanza ikiwa dhidi ya Kagera Sugar Agosti 17.
Mpaka sasa Azam imecheza michezo miwili ya kirafiki ikiwa kwenye kambi hiyo jijini El Gouna wakiwa wamefungwa mmoja dhidi ya Wadi Degla kwa bao 1-0 kabla ya kuifunga Grand SC kwa bao 1-0 lililowekwa kimiani na Prince Dube.
Kocha wa Azam, Abdihamid Moallin ameoneshwa kufurahishwa na muunganiko wa kikosi hicho chenye wachezaji wapya tisa, akisisitiza kuwa timu hizo walizocheza nazo zimewapa mwanga ndani ya timu yao katika maandalizi yao hayo.
Soka Watano Azam watua Misri
Watano Azam watua Misri
Related posts
Read also