London, England,
Mpango wa Man United kumsajili nyota wa Barcelona, Frenkie de Jong umeanza kuwa mgumu baada ya Chelsea nayo kudaiwa kuingia katika mbio hizo
Kwa kipindi kirefu kocha wa Man United, Erik ten Hag amekuwa akidaiwa kumtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye amewahi kuwa naye katika klabu ya Ajax na hivyo anataka kuungana naye kwa mara nyingine Man United.
Mpango huo hata hivyo unaonekana kuwa mgumu kwa sababu mbalimbali moja ni madai kwamba Barcelona imekuwa ikitaka fedha nyingi lakini pia kuna habari kwamba mchezaji huyo naye anaonekana kusita kujiunga na Man United huku Barcelona nayo inaonekana bado kuihitaji huduma yake na hapo hapo Chelsea naye imeingia katika mbio hizo hivyo kuiweka Man United katika wakati mgumu.
Na ingawa kocha wa Barcelona Xavi amesema kwamba hajui iwapo De Jong ataendelea kuwa na timu hiyo katika msimu wa 2022/23 lakini utayari wa klabu hiyo kumuachia unaonekana kuwa mgumu hasa kwa kuwa nayo inajitahidi kujiimarisha licha ya hali ngumu ya kiuchumi inayowakabili.
Barcelona tayari imetumia zaidi ya Euro 150 milioni kwa usajili wa Raphinha, Robert Lewandowski na Jules Kounde huku pia ikiwasajili Andreas Christensen na Franck Kessie waliokuwa wachezaji huru na ni wazi kwamba De Jong anahitajika katika mpango wa kuiimarisha timu hiyo licha ya madai ya Xavi kwamba hana uhakika wa kuendelea kuwa na mchezaji huyo.
Kimataifa Chelsea nayo yamtaka De Jong
Chelsea nayo yamtaka De Jong
Read also
