Barcelona, Hispania
Mshambuliaji mpya wa Barcelona, Robert Lewandowski aliyejiunga na timu hiyo hivi karibuni akitokea Bayern Munich ameishutumu klabu yake ya zamani kwa kusema uwongo kuhusu kuondoka kwake kwa lengo la kuwatuliza mashabiki.
Akizungumza katika mahojiano na chombo kimoja cha habari, Lewandowski aliulizwa sababu hasa iliyomfanya aihame Bayern kuwa ni uvumi ulioenea kwamba timu hiyo ilipanga kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Erling Haaland ambaye hata hivyo baadaye alijiunga na Man City.
“Hapana, hakuna uhusiano wowote na usajili wa Erling, mimi ni mtu ambaye hata kama jambo fulani si zuri kwangu ukweli unabaki kuwa muhimu, sitaki kuzungumzia nini hasa kilichotokea lakini kama sababu ya kuhama ni Erling, hiyo hapana, mimi sikuona tatizo lolote kama yeye angejiunga na Bayern Munich.
“Lakini kuna aina ya watu ambao hawasemi ukweli kuhusu mimi, wanasema vitu tofauti, lakini kwangu wakati wote ni muhimu kuwa wazi, kusema ukweli na labda kwa baadhi ya watu wachache hilo lilikuwa tatizo, ni sawa lakini mwisho wa siku niliona ni wakati sahihi kwa mimi kuondoka Bayern Munich na kujiunga na Barcelona,” alisema.
“Nilikuwa na uhusiano mzuri na wachezaji wenzangu, maofisa, kocha na haya yote ni mambo ambayo nitayakosa kwa sababu nilikuwa na wakati mzuri pale na hatukuwa marafiki uwanjani tu bali ilikuwa ni zaidi ya hivyo, lakini hatimaye ukurasa umefungwa na nafungua ukurasa mpya wa maisha yangu.”
“Kwa hiyo najiona niko katika msimamo sahihi, mahali sahihi lakini yote ambayo yalijitokeza mwishoni, wiki chache kabla sijaondoka Bayern Munich ni siasa nyingi, klabu ilikuwa inajaribu kutafuta hoja ya kwanini wanaweza kuniuza mimi katika klabu nyingine, kwa sababu hapo kabla labda kulikuwa na ugumu kulieleza hilo kwa mashabiki, na lazima nikubali kwamba kuna uwongo mwingi umesemwa kuhusu mimi, lakini yote kwa yote bado najua ukweli kwamba mashabiki hata katika wakati huu bado wananiunga mkono.
Lewandowski ameondoka Bayern baada ya kuichezea timu hiyo kwa mafanikio kwa miaka minane akifunga mabao 344 katika mechi 375, awali klabu yake ilikuwa ikipata tabu kumruhusu aondoke licha ya mwenyewe kusisitiza azma yake ya kutaka changamoto mpya kwingineko Ulaya.
Kimataifa Lewandowski: Bayern waongo
Lewandowski: Bayern waongo
Read also
