Na mwandishi wetu
Kipa Metacha Mnata amefikishwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kusaini katika klabu ya Singida Big Stars huku akidaiwa kuwa na mkataba wa mwaka mmoja na Polisi Tanzania.
Mwenyekiti wa Polisi Tanzania, Charles Mkumbo, amesema leo kuwa wameamua kwenda kushitaki TFF kupata hatma ya kipa huyo huku akieleza wazi kushangazwa na maamuzi ya Metacha kusaini Singida huku akitambua kuwa bado ana mkataba na Polisi.
Hayo yameibuka zikiwa zimepita wiki mbili tangu Singida imtambulishe rasmi kipa huyo wa zamani wa Yanga kabla ya Polisi nao kudai bado wana mkataba naye na kisha leo kueleza azma yao hiyo mpya.
“Tulishangaa kuona Metacha amekwenda kusaini Singida wakati akijua bado ana mkataba wa mwaka mmoja na sisi, tumeamua kuzingatia sheria na kanuni za soka ndiyo maana tumepeleka jambo hili TFF.
“Sasa baada ya hapo tutakuwa tukisubiri majibu ya TFF kuhusiana na Metacha, maana sisi tuna vielelezo vyote vinavyoonyesha ni mchezaji wetu halali,” alisema Mkumbo.
Hata hivyo, Singida ambayo pia imemsajili kipa wa Azam, Benedict Haule kupitia kwa mtendaji wake mkuu, Muhibu Kanu, naye aliwahi kukaririwa akisema kwamba wakati wanamsajili Metacha walipata uhakika kuhusu kuwa huru lakini kama kuna changamoto yoyote anaamini wanaweza kukaa mezani na kulimaliza suala hilo.
Soka Metacha Mnata ashtakiwa TFF
Metacha Mnata ashtakiwa TFF
Read also