Na mwandishi wetu
Beki wa kati wa Simba, Erasto Nyoni amesema licha ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza msimu uliopita na kulazimika kusugua benchi kwa kipindi kirefu hajakata tamaa hata kidogo badala yake yuko kamili kuendelea kupigania nafasi yake.
Nyoni ambaye ni kati ya wachezaji wakongwe katika kikosi cha Simba amekiri pia kushindwa kutimiza malengo yake mengi kama mchezaji lakini kwa kuwa bado yupo Simba anaamini msimu ujao atapambana kutimiza mengi anayoyapanga akiwa katika kikosi cha timu hiyo.
“Msimu uliopita kwetu ulikuwa mbaya sana, hatukufanya vizuri, hatukutimiza malengo tuliyojiwekea, mpaka tunamaliza tumeshindwa kufanikisha malengo, kwa kifupi msimu ulikuwa mgumu na mbaya kwetu sisi.
“Lakini binafsi pia nilikuwa na changamoto ya kukosa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza, vile vile kupata nafasi hata ya dakika 30, 20 ilikuwa ngumu kwangu kuipata, kikubwa sikukata tamaa, nikapambana nikapata nafasi ya mechi za kukamilisha ratiba, tukamaliza vizuri na hiyo haijanikatisha tamaa bado napambana.
“Sikuwa na furaha pia msimu uliopita kwa sababu sikutimiza malengo yangu ndani ya klabu, kwa sababu hii ni kazi yangu, msimu unapoanza unajiwekea malengo kwa hiyo msimu unapoisha bila kufanikisha malengo inaumiza, hakukwa na kilichonifurahisha,” alisema Nyoni.
Pamoja na hayo, Nyoni anayemudu pia kucheza kama kiungo anatarajia kukutana na changamoto nyingine mpya baada ya kutua kwa beki Muivorycoast, Mohamed Outtara. Mabeki wengine wa eneo hilo ni Inonga Baka, Joash Onyango na Kennedy Juma.
Soka Benchi halijamkatisha tamaa Nyoni
Benchi halijamkatisha tamaa Nyoni
Read also
