Na mwandishi wetu
Kikosi cha Azam kimeondoka nchini leo kuelekea El Gouna, Misri kwa ajili ya kuweka kambi ya siku 20 ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara utakaofunguliwa Agosti 17, mwaka huu.
Msafara wa Azam umejumuisha wachezaji 28 na viongozi sita wa benchi la ufundi. Wachezaji waliondoka ni makipa Ali Ahamada, Wilbol Maseke, Ahmed Salula na Zuberi Foba, mabeki ni Abdallah Kheri, Daniel Amoah, Malickou Ndoye, Twalib Mohamed, Bruce Kangwa, Edward Manyama na Nathaniel Chilambo.
Viungo ni Keneth Muguna, Sospeter Bajana, Isah Ndala, Idd Seleman, Kipre Junior, Tepsie Evance, Ibrahim Ajibu, Cleophace Mkandala, Tape Edinho, James Akaminko, Ayoub Lyanga, Ismail Aziz huku washambuliaji ni Shaaban Idd, Idris Mbombo, Rodgers Kola na Prince Dube.
Ofisa Habari wa Azam, Thabiti Zacharia alisema kuwa lengo kubwa la kwenda kuweka kambi nchini Misri ni kuipa timu utulivu na kuitafutia michezo ya kirafiki ambayo itakuwa kipimo cha ubora wa kikosi chao.
“Naamini zitakuwa siku 20 za kambi yetu ya Misri itakayoenda kuwajenga zaidi wachezaji wetu wapya lakini pia ni muda mwafaka kwa kocha kutengeneza kikosi na kupata muunganiko mzuri kikosini kwa ajili ya michuano tutakayoshiriki msimu ujao,” alisema Zachakaria.
Azam ambayo msimu uliopita imemaliza kwenye nafasi ya tatu, imekata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ikionyesha kupania kutanua makucha yake katika michuano hiyo sanjari na ile ya Ligi Kuu ya NBC.
Soka Azam haoo Misri
Azam haoo Misri
Related posts
Read also