Na mwandishi wetu Tanzania Prisons ipo kwenye mchakato wa kupunguza takriban wachezaji wanane hadi tisa kwa ajili ya kuiweka sawa timu hiyo kuelekea msimu ujao ili yasijirudie yaliyowakuta msimu wa 2021/22 uliomalizika hivi karibuni.
Prisons imenusurika ko ushuka daraja baada ya kucheza mechi nne za mtoano kutokana na kufanya vibaya Ligi Kuu Bara msimu wa 2021/2022.
Kwanza ilicheza na Mtibwa Sugar ambapo ilifungwa mabao 3-2 ikiwa ni matokeo ya mechi za nyumbani na ugenini, kisha ikavaana na JKT Tanzania ya Championship kujitetea kwa mara ya mwisho ambapo walifanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla wa mabao 2-1 wa mechi ya nyumbani na ugenini na kusalia Ligi Kuu msimu ujao.
Sasa katika mpango wake wa kuweka mambo sawa, kocha msaidizi wa timu hiyo, Shaban Mtupa ameeleza miongoni mwa mipango waliyonayo kuhakikisha wanafanya vizuri msimu ujao ni pamoja na kupunguza idadi ya wachezaji hao na kuongeza takriban 10 wapya.
“Sikatai wapo waliopambana mno ndiyo maana tumebaki Ligi Kuu lakini ili kuhakikisha hayatokei tena haya yaliyotokea sasa hivi ni lazima tuongeze wachezaji takriban 10 na watapungua wachezaji nane mpaka tisa.
“Kingine ni kushindwa kuwa na maandalizi mazuri ya msimu ujao ambapo hilo lilianza kutuvuruga tangu tunaanza ligi msimu uliopita na kushindwa kupata matokeo mapema na kuja kuteseka mwishoni, tutahakikisha haturudii tena kilichotupata sasa,” alisema Mtupa.
Soka Prisons kuacha wachezaji wanane
Prisons kuacha wachezaji wanane
Related posts
Read also