Milan, Italia
Klabu ya soka ya AC Milan ya Italia imemsajili mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Divock Origi kwa mkataba unaofikia ukomo Juni 2026.
Origi, Mkenya mwenye uraia wa Ubelgiji amejiunga na vigogo hao wa Italia akiwa mchezaji huru na amechukua uamuzi wa kuikimbia Liverpool kwa kinachoaminika na wengi kuwa ni kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza cha Liverpool.
Akiwa Liverpool pamoja na kuwa na nafasi ndogo ya kucheza lakini mara kadhaa amekuwa akiitumia nafasi hiyo vizuri kwa kuipa Liverpool ushindi, mfano Aprili 2018 anakumbukwa alipotokea benchi na kufunga bao muhimu katika dakika tano za nyongeza katika mechi ngumu ya Liverpool dhidi ya mahasimu wao Everton, bao lililompagawisha kocha Jurgen Klopp na kuipa Liverpool ushindi wa 2-0.
Pia Origi anakumbukwa kwa bao lake kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2019 pamoja na mabao yake mawili katika ushindi wa mabao 4-0 ambao Liverpool iliupata dhidi ya Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliofuata.
Anaondoka Liverpool akiwa ameifungia timu hiyo jumla ya mabao 41 katika mechi 175 lakini kubwa ni rekodi yake ya kufunga mabao 11 akitokea kwenye benchi na sasa anajiunga na vigogo hao wa Milan wanaonolewa na kocha Stefano Pioli.
Kimataifa Origi asaini AC Milan
Origi asaini AC Milan
Related posts
Read also