Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Peter Banda ametajwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuwa miongoni mwa wachezaji makinda bora waliofanya vizuri kwenye ngazi ya mashindano ya klabu ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliomalizika wa 2021-22.
Banda raia wa Malawi mwenye miaka 21 ametajwa sambamba na makinda wengine watatu ambao ni Mkongo Guy Mbenza, 22 anayekipiga kwa mkopo Wydad Casablanca akitokea Royal Antwerp ya Ubelgiji aliyokuwa akiichezea Mbwana Samatta ambaye naye alikuwa kwa mkopo hapo akitokea Fenerbahçe ya Uturuki.
Wawili wengine ni kiungo mshambuliaji Ahmed Abdelkader, 23 anayeitumikia Al Ahly ya kwao Misri na winga wa kushoto wa RS Berkane, Mouad Fekkak, 22 raia wa Morocco.
Banda ambaye ametua Simba msimu huu akitokea Big Bullets ya kwao Malawi baada ya kumaliza kuitumikia FC Sheriff ya Moldova kwa mkopo wa miezi sita ameifungia Simba bao moja kwenye mechi saba za michuano hiyo kati ya nane ilizocheza huku akionesha kiwango kikubwa na cha kuvutia licha ya kutomaliza dakika 90 kwenye mechi hata moja.
Simba iliishia kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufungwa na Orlando Pirates ya Afrika Kusini kwa matuta 4-3 baada ya kila timu kushinda bao 1-0 ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani.
Soka Banda ang’ara CAF
Banda ang’ara CAF
Related posts
Read also