Na mwandishi wetu
Klabu ya Azam FC imeendelea kushusha vifaa vipya kwa ajili ya msimu ujao kwa kumtambulisha kiungo mwingine mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Tape Edigno aliyesaini jana mkataba wa miaka mitatu na timu hiyo.
Edigno ni mchezaji wa pili wa Ivory Coast Azam inamtambulisha kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya NBC, baada ya awali kumtambulisha kiungo mwingine, Kipre Junior kutoka Sol FC ya kwao kwa kandarasi ya miaka mitatu pia.
Azam imemtambulisha mchezaji huyo anayetajwa kufunga mabao matano na asisti tisa kwenye Ligi Kuu ya Ivory Coast (Ligue 1) mbele ya Mmiliki wa Azam, Yusuf Bakhresa na Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Abdulkarim Amin ‘Popat’.
Ni kama vile mwendelezo wa kauli iliyotolewa awali na Bakhresa kupitia kurasa za mitandao yake ya kijamii kuwa sasa ameamua kuwafurahisha mashabiki wa Azam kwa kushusha ‘vyuma’ baada ya vyuma kuelekea msimu ujao.
Timu hiyo iliyomaliza nafasi ya tatu msimu huu, msimu ujao itashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hivyo inajiweka sawa mapema pia kwa ajili ya kuongeza ushindani kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu ya NBC kutokana na ushindani walioupata msimu huu kiasi cha kugombania nafasi ya tatu zikiwa zimesalia mechi chache kabla ya kumalizika kwa ligi.
Soka Azam yashusha kifaa cha pili
Azam yashusha kifaa cha pili
Related posts
Read also