London, England
Mapema mwezi huu, Cristiano Ronaldo alishauri kocha mpya wa Man United, Erik ten Hag apewe muda lakini huenda amejipima na kuona hana nafasi katika timu hiyo hivyo ameanza mipango ya kuondoka.
Habari za ndani kutoka katika klabu hiyo zinadai kwamba Ronaldo amejiangalia na kujiona hayumo katika mipango ya baadaye ya Ten Hag katika kikosi cha Man United hasa kwa kuzingatia aina ya mfumo anaoutaka kocha huyo.
Inadaiwa kwamba wakala wa mchezaji huyo, Jorge Mendes ameingia msituni akimtafutia Ronaldo timu nyingine barani Ulaya huku kukiwa na habari kwamba klabu mbili tayari zimeonyesha nia ya kutaka huduma ya mchezaji huyo ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 37.
Klabu ya kwanza inayotajwa ni Roma inayonolewa na Jose Mourinho ambaye amewahi kuwa na Ronaldo katika klabu ya Real Madrid ya Hispania na ya pili ni Sporting CP ya Ureno, klabu ambayo alianza kuichezea katika timu ya vijana kabla ya kuondoka na kujiunga na Man United mwaka 2003.
Katika msimu wa 2021/22, licha ya umri wake kuwa mkubwa, Ronaldo alitamba katika upachikaji mabao Man United akifunga jumla ya mabao 24 katika mechi 37 na kumaliza msimu akiwa kinara wa mabao kwa timu hiyo.
Rekodi hiyo si mbaya kwa mchezaji wa umri wake na ingawa Ten Hag hajasema lolote kuhusu mchezaji huyo, kinachoonekana ni kama vile Ronaldo amejipima na kuiona nafasi yake ndogo na kwa kuwa anaamini katika uwezo wake haishangazi kuanza mipango ya kuondoka.
Kimataifa Ronaldo ataka kuondoka Man United
Ronaldo ataka kuondoka Man United
Related posts
Read also