Na mwandishi wetu
Baada ya kutambulishwa rasmi jana na klabu yake mpya ya Simba, mshambuliaji Moses Phiri anatarajia kurejea kwao Zambia kesho kwa lengo la kujiweka sawa kabla ya kurejea nchini baadaye.
Phiri ametambulishwa na kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia timu hiyo ya mitaa ya Kariakoo, Msimbazi, Dar es Salaam akitokea Zanaco FC ya Zambia ambako alionesha kiwango kikubwa.
Meneja wa Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally ameeleza kwamba wamemalizana vizuri na mchezaji huyo mpaka timu yake ya Zanaco ndiyo maana hawakuona shida kumtambulisha kipindi hiki licha ya kuelezwa kuwa angemalizana na Zanaco mwisho wa mwezi Juni, mwaka huu.
“Kila kitu kilikwenda vizuri ndiyo maana tumemtambulisha sasa, tumemalizana na mchezaji mwenyewe ndiyo maana tumelifanya hilo suala kuwa rasmi jana, nieleze tu kuwa watu wasiwe na haraka kujua nani atafuata ila wakae sawa hivi karibuni tutatangaza mwingine.
“Lakini kabla ya Phiri kuondoka kurejea kwao kesho, leo atahudhuria na kuungana na wenzake kwenye Uwanja wa Mkapa kuishuhudia timu ikipambana na Mbeya City kisha baada ya hapo atarajea kwao na atarudi nchini wakati wa kuanza maandalizi ya msimu mpya,” alisema Ally.
Phiri mwenye miaka 29, kabla ya kutua Simba amewahi kukipiga Buildcon FC ya Zambia pia Academico Viseu na S.C. Covilhã za nchini Ureno.
Soka Phiri wa Simba arudi kwao
Phiri wa Simba arudi kwao
Related posts
Read also