Na mwandishi wetu
Wakati klabu ya Yanga ikielekea kwenye uchaguzi mkuu, wanachama wa klabu hiyo wametakiwa kuhakikisha wanakamilisha taratibu zote kikatiba ili wapeta fursa ya kupiga kura ya kuchagua kikamilifu viongozi wao wapya.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Yanga, Malangwe Mchungahela kuelekea kwenye uchaguzi huo unaotarajia kufanyika Julai 10, mwaka huu.
Uchaguzi huo kwa sasa uko katika mchakato wa kupokea mapingamizi baada ya kukamilika kwa zoezi ya urudishwaji wa fomu na kupitia majina ya wagombea na baadaye kamati hiyo kutoa majina ya wagombea waliokidhi vigezo na kuendelea na mchakato unaofuata.
Mchungahela amebainisha kuwa mpaka sasa taratibu zote zinazohusiana na uchaguzi huo zinakwenda vizuri na hawajapokea pingamizi lolote kuhusu mgombea wa nafasi yoyote.
“Hii inaonesha kazi ya upembuzi kwa wagombea imefanyika kwa weledi mkubwa na hivyo ndivyo tulivyotaka sababu lengo ni kuhakikisha uchaguzi huu unafanyika kwa amani na uwazi ili kila mtu akapate haki yake,” alisema Mchungahela.
Kiongozi huyo alisema kuwa kwa sasa hawawezi kujua idadi kamili ya wanachama watakaoshiriki kupiga kura sababu bado chaguzi za matawi hazijamalizika lakini anaamini jambo hilo linakwenda vizuri na muda sio mrefu utakamilika na kamati yake itapata idadi kamili ya wapiga kura.
Nafasi zinazogombewa kwenye uchaguzi huo ni Rais wa klabu ambayo ina mgombea mmoja pekee, Injinia Hersi Said wakati nafasi ya Makamu wa Rais inawaniwa na Arafat Haji na Suma Mwaitenda huku nafasi za wagombea ujumbe zikiwa na idadi kubwa ya wagombea jambo linaloonesha kutakuwa na ushindani mkubwa katika nafasi ya ujumbe.
Soka Kamati ya uchaguzi Yanga yatoa angalizo
Kamati ya uchaguzi Yanga yatoa angalizo
Related posts
Read also