London, England
Kiungo mkongwe wa Manchester United, Cristiano Ronaldo amesema anaamini timu hiyo itapata mafanikio chini ya kocha mpya, Erik ten Hag huku akitaka kocha huyo apewe muda.
Kauli hiyo ya Ronaldo imekuja wakati ambao timu hiyo ina kumbukumbu ya msimu ulioisha hivi karibuni ambao umekuwa wa hovyo ikimaliza na pointi 58 na kushindwa kufuzu fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Ronaldo hata hivyo ni kama vile anaamini yaliyopita yamepita na kwa sasa anasema kwamba anajiandaa kwa msimu ujao akiwa tayari kuisaidia timu hiyo kurudi mahala pake.
“Ni kweli kwamba nilikuwa mwenye furaha kurudi katika klabu hii ambayo kwa hakika imenisaidia kukuza kiwango changu katika soka, kwa hiyo ni jambo ambalo usingeweza kuamini,” alisema Ronaldo.
“Lakini jambo la muhimu kwangu ni kujaribu kushinda mechi na kushinda mataji au makombe mengine, bado naamini Manchester itarudi mahala pake, kuna wakati inachukua muda lakini imani hiyo bado ninayo,” alisema.
Akifafanua kuhusu Ten Hag, kocha Mholanzi aliyeshinda mataji matatu ya Ligi Kuu Uholanzi akiwa na klabu ya Ajax, Ronaldo alisema kwamba kocha huyo anahitaji muda ili kupata mafanikio England.
“Najua alifanya kazi nzuri akiwa Ajax na kwamba ni kocha mzoefu lakini tunahitaji kumpa muda na mambo yanahitaji kubadilika kwa namna anavyotaka yeye.
Soka Ronaldo: Ten Hag apewe muda Man Utd
Ronaldo: Ten Hag apewe muda Man Utd
Related posts
Read also