London, England
Kocha wa Everton, Frank Lampard ametozwa faini ya Pauni 30,000 (Ssh 90 milioni za Tanzania) na Chama cha Soka Engand (FA) kutokana na kauli aliyoitoa dhidi ya waamuzi.
Baada ya timu yake kufungwa mabao 2-0 na Liverpool katika mechi iliyopigwa mwezi uliopita, Lampard alionyesha kukerwa na kitendo cha mwamuzi Stuart Attwell kutoipa timu yake penalti baada ya Joel Matip kumchezea rafu Anthony Gordon.
Taarifa ya FA ilidai kuwa Lampard alivunja sheria namba E3 inayohusu maoni ya kwenye vyombo vya habari ingawa pia waliwasilisha malalamiko yao kwa baada ya mechi hiyo wakihoji ni kwa nini rafu aliyofanyiwa Gordon haikupitiwa kwa mara nyingine.
Rafu aliyochezewa Gordon ilitokea wakati timu hizo zikiwa hazijafungana lakini dakika nane baadaye Andy Robertosn aliifungia Liverpool bao la kwanza kabla Divock Origi hajaongeza la pili na la ushindi kwa timu hiyo.
“Ile ilikuwa ni penalti lakini huwezi kuipata Anfield, kama ingekuwa ni Mohamed Salah kwenye eneo lao naamini mwamuzi angetoa penalti, ile ni rafu alifanyiwa Anthony.”
Baadaye ilielezwa kuwa kauli ya Lampard ilimaanisha kwamba penalti ingetolewa kama kosa lile angefanyiwa mchezaji wa Liverpool.
Kimataifa FA yampiga rungu Lampard
FA yampiga rungu Lampard
Related posts
Read also