Na mwandishi wetu
Kiungo wa Simba, Clatous Chama amesema amesahau yaliyopita na yupo nchini kwa ajili ya kuitumikia na kuipa mataji timu hiyo bila kinyongo.
Akizungumza na GreenSports, mchezaji huyo alisema anatambua maneno mengi yamesemwa kutokana na adhabu ya kusimamishwa na timu hiyo kwa utovu wa nidhamu, lakini anaushukuru uongozi wa Simba kwa kukubali msamaha wake.
“Nipo hapa kwa ajili ya kuipigania Simba kubeba mataji katika mashindano yote, changamoto za hapa na pale ni vitu vya kawaida kwenye kazi, nafurahi yamepita na sasa nipo kazini,” alisema Chama.
Kiungo huyo alisema hataki kuendeleza malumbano ambayo hayana msingi sababu suala la msingi lilishamalizika na yupo kazini.
Chama alisimamishwa na uongozi wa timu hiyo pamoja na Nassoro Kapama kwa madai ya utovu wa nidhamu lakini baadaye yeye alirudishwa kundini baada ya kuomba msamaha kwa viongozi na benchi la ufundi la timu yake.
Soka Chama asahau yaliyopita
Chama asahau yaliyopita
Read also