Na mwandishi wetu
Sare ya bao 1-1 na Singida Big Stars imetosha kuifanya Yanga iungane na mahasimu wao Simba kwa kutolewa katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar.
Kwa matokeo hayo, Singida Big imetinga hatua ya nusu fainali na inasubiri kuumana na Azam katika mechi itakayopigwa kesho Jumapili ambapo mshindi atakuwa amefuvu moja kwa moja hatua ya fainali dhidi ya mshindi wa mechi ya Namungo na Mlandege.
Singida Big ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuliona lango la Yanga kwa bao lililofungwa na Kazadi Kasengu baada ya kuuwahi mpira wa kona uliotemwa na kipa wa Yanga kabla ya Yanga kusawazisha kwa mpira wa adhabu uliopigwa na beki wa kushoto wa timu hiyo, David Bryson.
Soka Yanga nayo yaaga Mapinduzi
Yanga nayo yaaga Mapinduzi
Related posts
Read also