Na mwandishi wetu
Mshambuliaji mpya wa Simba, Saido Ntibazonkiza kwa mara ya kwanza ameeleza furaha yake ya kutua Simba huku akiahidi makubwa kwa mashabiki wa timu hiyo.
Saido ambaye ametua Simba hivi karibuni akitokea Geita Gold, amesema kwa ukubwa na uzoefu wa wachezaji wa Simba aliowakuta anaamini hiyo itamsaidia kuwika mno zaidi ya hata alipokuwa akiichezea Geita.
Mchezaji huyo raia wa Burundi msimu huu amefanikiwa kufunga mabao manne na kutoa pasi za mabao sita akizidiwa pasi tatu na kinara Clatous Chama wa Simba.
“Kwa jinsi Simba ilivyo, ina wachezaji wakubwa, wazuri, wazoefu pia naamini watanisaidia kwa kiasi kikubwa na hiyo itanifanya niisaidie timu na nitafanya vizuri zaidi ya nilipokuwa Geita maana huu ni mwaka wa pili sasa nipo hapa Tanzania, nawajua wachezaji wa Simba.
“Wengine ni rafiki zangu wa muda mrefu kina Erasto (Nyoni), Mkude (Jonas), natamani kucheza nao kama vile ambavyo huwezi kuficha juu ya kiwango cha Chama na wachezaji wengi wanatamani kucheza naye, wapo wengi Simba wako vizuri nafikiri tusiongee sana tusubiri miguu itaamua,” alisema Saido.
Kabla ya kuichezea Geita, Ntibazonkiza aliwahi kukipiga Vital’O ya Burundi, SM Caen ya Ufaransa, Cracovia ya Poland na nyingine pia kabla ya kutua Yanga msimu wa 2020-21.
Soka Ntibazonkiza aahidi makubwa Simba
Ntibazonkiza aahidi makubwa Simba
Related posts
Read also