Barcelona, Hispania
Kocha wa Barcelona, Xavi Hernandez amekubali ukweli kwamba anaweza kupoteza kazi wakati wowote kama hatoshinda mataji msimu huu hasa baada ya kupitia katika wiki ngumu.
Barca ikiwa nyumbani Nou Camp wiki iliyopita ililazimisha sare ya mabao 3-3 dhidi ya Inter Milan na hivyo huenda ikatolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iwapo Inter itaifunga Viktoria Plzen katika mechi ya mwisho ya hatua ya makundi. Ikitokea hali hiyo Barca itakuwa imeaga michuano hiyo katika hatua ya makundi mara ya pili mfululizo.
Timu hiyo pia Jumapili iliyopita ilikubali kichapo cha mabao 3-1 mbele ya mahasimu wao Real Madrid katika mechi ya La Liga hali ambayo iliendelea kuzua hofu kuhusu hatima ya Xavi.
“Ni kweli naweza kufukuzwa kazi, lakini hadi sasa hakuna aliyeniambia lolote,” alisema Xavi kwenye mkutano na waandishi wa habari hii leo Jumatano alipoulizwa kama ataelewa iwapo klabu hiyo itapoteza imani naye.
“Hii ni Barca, kwa juhudi zilizofanywa na klabu (katika usajili) na kikosi tulichonacho ni lazima tupiganie mataji na tusiposhinda ni kama rais alivyowahi kusema kwamba kuna kitakachofuata na kitaanzia kwangu,” alisema Xavi.
“Hata hivyo nitafanya kila liwezekanalo ili kazi iwe na mafanikio, wakati wowote naweza kukosa sapoti ya klabu, hata kesho, hili ni soka, tumepoteza mechi dhidi ya Madrid, tuko mguu ndani mguu nje kwenye Ligi ya Mabingwa lakini wakati wote mimi nina msimamo chanya,” aliongeza Xavi.
Katika hatua nyingine, Xavi alisema kwamba alijiona kama mtu ambaye amepoteza rafiki wa karibu wa familia kutokana na ujumbe ambao amekuwa akitumiwa baada ya mambo kwenda vibaya katika mechi dhidi ya Inter Milan na baadaye dhidi ya Madrid.
Kimataifa Xavi: Naweza kutimuliwa Barca
Xavi: Naweza kutimuliwa Barca
Related posts
Read also