London, England
Mechi ya Europa Ligi kati ya Arsenal na PSV Eindhoven imeahirishwa sababu ikielezwa kuwa ni uchache wa watu wa usalama kutokana na shughuli za msiba wa Malkia Elizabeth 11.
Mechi hiyo ilipangwa kuchezwa Alhamisi kwenye Uwanja wa Emirates lakini kutokana na msiba wa Malkia Elizabeth 11 imeonekana kiusalama mechi hiyo ni vyema kuahirishwa na tayari Uefa wameahidi kutangaza siku nyingine ya kuchezwa mechi hiyo.
Awali kulikuwa na wasiwasi kwamba huenda mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Chelsea na Red Bull Salzburg iliyopangwa kuchezwa Jumatano kwenye Uwanja wa Stamford Bridge ingeahirishwa lakini taarifa za awali zinadai kwamba mechi hiyo itachezwa kama kawaida.
Taarifa ya Uefa ya kuahirisha mechi ya Arsenal ilieleza, “Hii ni kwa sababu za kiusalama na maandalizi ya mechi hiyo kuingiliana na shughuli za maandalizi ya msiba wa Malkia Elizabeth.
Uefa pia walishatangaza kuahirisha mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Rangers na Napoli iliyokuwa ichezwe Jumanne na sasa itachezwa Jumatano sababu ikiwa ni hizo hizo za kiusalama na muingiliano wa shughuli za msiba wa Malkia Elizabeth 11 ambaye anatarajia kuzikwa Jumatatu ijayo.
Tofauti na hivyo mechi Tottenham ambayo itakuwa ugenini dhidi ya Sporting Lisbon, mechi hiyo itachezwa Jumanne kama kawaida kama ilivyo kwa mechi kati ya Liverpool watakaokuwa wenyeji wa Ajax ambayo pia kama kawaida itachewa Jumanne kama ambavyo Celtic nayo itasafiri hadi Poland kuikabili Ajax Jumatano.
Mechi nyingine ambazo zitachezwa kama kawaida ni mechi kati ya Manchester City na Borussia Dortmund ambayo itapigwa Jumatano sawa na mechi ya Europa Ligi ya Manchester United ambayo itakuwa ugenini dhidi ya Sheriff Tiraspol siku ya Alhamisi.
Kimataifa Mechi ya Arsenal, PSV yaahirishwa
Mechi ya Arsenal, PSV yaahirishwa
Related posts
Read also