London, England
Kocha wa Tottenham Hotspur, Antonio Conte amesema klabu ya Bayern Munich inawakosea heshima kwa kuzungumzia uwezekano wa kumsajili Harry Kane kwa siku zijazo.
Hivi karibuni gazeti maarufu nchini Ujerumani la The Bild lilizungumzia taarifa ya wawakilishi wa Kane ambao walisema kwamba hawawezi kuufuta uwezekano wa mchezaji huyo kujiunga na Bayern jambo ambalo limemchukiza Conte.
Kane msimu uliopita alionekana kutaka kuondoka Spurs na kujiunga na Man City lakini mpango huo ulikwama na baada ya hapo akabaki kuwa mchezaji muhimu wa timu hiyo akifunga mabao 17 katika mechi 37 za Ligi Kuu England na kuisaidia timu hiyo kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mpango wa Bayern kutaka kumsajili Kane umekuja wakati huu kwa kinachoaminika kuwa klabu hiyo inahitaji mshambuliaji wa kuiongezea nguvu safu yao ya ushambuliaji baada ya kuondoka kwa Robert Lewandowski ambaye amejiunga na Barcelona.
Akizungumza jana baada ya Spurs kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya kirafiki ya kujiandaa na msimu wa 2022/23, mechi ambayo Kane alifunga mabao yote mawili, Conte alielezea namna anavyokerwa na Bayern kuzungumza hadharani kuhusu mshambuliaji wake.
“Sijui kwa nini Kane anahusishwa na Bayern, suala hili liko wazi kwa Tottenham na Harry, ni mtu muhimu katika mpango wetu, mimi huwa sipendi kumzungumzia mchezaji wa timu nyingine, labda hilo ni kuikosea heshima klabu nyingine,” alisema Conte.
Kauli hiyo ya Conte imekuja baada ya mmoja wa vigogo wa Bayern, Julien Nagelsmann kusema kwamba Kante ambaye amebakisha miaka miwili katika mkataba wake na Spurs atakuwa mtu fiti sana kwa Bayern.
“Tatizo ni kwamba ni mchezaji ambaye ada yake iko juu sana, lakini ni mahiri, ni kati ya wachezaji wawili au watatu wanaoweza kucheza nafasi ya mshambuliaji wa kati, ana nguvu, mahiri kwa kutumia kichwa na miguu yote,” alisema Nagelsmann.
“Anaweza kufunga mabao mengi akiwa Bundesliga (Ligi Kuu Ujerumani) siijui bei yake lakini ni ngumu mno kwa Bayern Munich, tutajua itakuwaje siku zijazo,” alisema Nagelsmann wakati ofisa mtendaji mkuu wa Bayern, Oliver Kahn yeye alisema Kane ni mshambuliaji wa hadhi ya juu duniani na kwamba mpango wowote wa uhamisho unaweza kufanywa siku zijazo, kauli ambazo zimemkera Conte.
Kimataifa Bayern wamchefua Conte
Bayern wamchefua Conte
Related posts
Read also