Na mwandishi wetu
Timu ya Singida Big Stars imeeleza kwamba inatarajia kurejea kuanza kambi ya maandalizi kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara 2022/23 mnamo Julai 10, mwaka huu.
Big Stars ambayo imepanda kushiriki Ligi Kuu ya NBC pamoja na Ihefu imefunguka kuwa taarifa hiyo ya kujumuika na timu tarehe hiyo ni kwa wachezaji wote na watakutana Dar es Salaam kisha watapangiwa ratiba nzima inakuwaje.
Mtendaji Mkuu wa Big Stars, Muhibu Kanu amesema leo kuwa wameshajua watakwenda wapi kuweka kambi na ratiba nyingine isipokuwa kwa sasa hawako tayari kuweka wazi mpaka timu nzima itakapokutana.
“Tunaendelea na ratiba nyingine kama kawaida licha ya kuendelea na usajili wa kuimarisha kikosi chetu, kwa hiyo tunatarajia kukutana tarehe 10 Julai, kituo kikiwa ni Dar es Salaam, wachezaji wote watakutana hapo.
“Na baada ya hapo ndipo utakapotoka utaratibu wa ratiba na wapi tunakwenda kufanya maandalizi yetu kama ni nje ya nchi au ni wapi,” alisema Kanu.
Timu hiyo ambayo awali ilifahamika kama DTB mpaka sasa imekamilisha usajili wa wachezaji watatu wapya ambao ni beki Paul Godfrey ‘Boxer’ kutoka Yanga, kiungo Aziz Andambwile (Mbeya City) na Kelvin Sabato (Mtibwa Sugar).
Soka Singida Big kambini Julai 10
Singida Big kambini Julai 10
Related posts
Read also