Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa Yanga, Saido Ntibazonkiza ameibuka na kusema kuwa anachafuliwa jina lake na atatoa tamko baada ya kumalizika kwa mechi ya Jumamosi baina ya Yanga na Simba.
Saido amezungumza hayo ikiwa ni siku moja imepita tangu yeye na mshambuliaji mwenzake, Dickson Ambundo kusimamishwa na kuondolewa kwenye kikosi cha timu hiyo kilichoweka kambi Shinyanga kujiandaa na mechi hiyo ya hatua ya musu fainali ya Kombe la Azam (ASFC) dhidi ya Simba.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, mshambuliaji huyo raia wa Burundi ameeleza kusikitishwa na kutokubali kuchafuliwa jina lake na kusisitiza ni kwa kiasi gani anafahamu umuhimu wa mechi hiyo, hivyo baada ya mechi hiyo atazungumza kinachoendlea.
“Uongo hutembea kwa kasi na ukweli huchelewa kufika. Kamwe sitaruhusu mtu yeyote kulichafua jina langu, baada ya mechi nitaongea Inshaallah. Nafahamu sana umuhimu wa mechi ya Jumamosi na kwa nguvu za Allah tutapata ushindi. Naipenda sana Yanga, Yanga tamu,” aliandika Sadio aliyewahi kukipiga SM Caen ya Ufaransa.
Yanga imelitolea ufafanuzi suala hilo kuwa wachezaji hao walifanya utovu wa nidhamu kwa kuondoka na kurudi alfajiri mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Biashara United, kitendo kilichomfadhaisha kocha Nassredine Nabi na kuamua kuwaondoa kambini wachezaji hao na amepanga kuzungumza nao kwa kina baada ya kumalizika kwa mechi hiyo itakayopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Soka Ntibazonkiza adai anachafuliwa jina
Ntibazonkiza adai anachafuliwa jina
Related posts
Read also