Na mwandishi wetu
Klabu ya Simba leo imemtangaza Imani Kajula (pichani) kuwa Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu hiyo kwa kipindi cha miezi sita akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Barbara Gonzalez.
Kajula amechukua nafasi hiyo ikiwa imepita takriban wiki tatu tangu kung’atuka kwa Barbara aliyetangaza azma yake hiyo tangu Desemba mwaka jana akieleza kuwa anapisha safu mpya ya uongozi kuwa huru kuchagua mtendaji wanayetaka kwenda naye.
Simba kwa sasa iko kwenye mchakato wa uchaguzi wa viongozi wapya wa miaka minne ijayo baada ya viongozi wa sasa kumaliza muda wake huku zikisalia siku mbili kabla ya kufanyika kwa uchaguzi Januari 29, mwaka huu.
Tangu Simba iingie kwenye mfumo mpya wa uendeshaji timu, Kajula anakuwa Mtendaji Mkuu wa tatu kwa klabu hiyo baada ya watangulizi wake Barbara na Senzo Mbatha raia wa Afrika Kusini.
Kajula mbali na kuwa mwanamichezo na mpenzi wa Simba lakini amewahi kufanya kazi katika mabenki ya CRDB na NMB akishika nafasi za meneja idara ya masoko.
Soka Kajula CEO mpya Simba
Kajula CEO mpya Simba
Read also