Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Suleiman Serera (pichani) amelitaka Baraza la Michezo la Taifa (BMT) liwe na mipango kabambe na imara itakayofanikisha ukuwaji na maendeleo ya michezo nchini.
Serera ametoa kauli hiyo alipokutana na kufanya mazungumzo na menejimenti ya baraza hilo ambapo amewataka waendelee kuimarisha ushirikiano na Serikali za Mitaa.
Alisema kwamba kwa kufanya hivyo watakuwa wanapeleka ujuzi na hamasa zaidi ya michezo kwa lengo la kuibua vipaji na kuimarisha afya za Watanzania kwa ujumla.
“Hatuwezi kufanikiwa kwenye eneo la michezo kama hatujashuka kwenye Serikali za Mitaa, hamasa huko chini ni kubwa ila inahitaji muunganiko mzuri na ushawishi kwa ajili ya kuibua na kuendeleza michezo kote nchini katika ufanisi mkubwa zaidi,” alisema Serera.
Serera alisisitiza zaidi kwa kulitaka baraza hilo kuhamasisha wananchi juu ya umuhimu wa michezo katika jamii ili kupambana na magonjwa yasiyoambukiza.
Kikao hicho kilikuwa cha kwanza kai ya Dk Serera na BMT, tangu kuteuliwa kwake katika nafasi hiyo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan.
Sports Mix Katibu awapa neno BMT
Katibu awapa neno BMT
Read also