Na mwandishi wetu
Imebainika kuwa muda mfupi ujao baadhi ya mechi za Ligi Kuu NBC zitaanza kuamuliwa kwa usaidizi
wa teknolojia ya video ya waamuzi (VAR).
Hayo yameelezwa lumamosi hii na Rais wa TFF, Wallace Karia akifafanua kuwa huo ni uamuzi waShirikisho la Soka Afrika (CAF), kuipa Tanzania vifaa vya VAR ambavyo vitafungwa katika baadhi yaviwanja.
Karia akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa TFF unaofanyika Iringa, alisema: “Niwape habari njema kuwa tumepata VAR kutoka CAF na hii ni mwendelezo wa uhusiano mzuri na CAF. Wataalamu wameingia jana (juzi) kutoa mafunzo. Itafungwa katika viwanja vyenye ubora.”
Karia alisema kuwa wanaangalia pia uwezekano wa VAR kufungwa katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar ikiwa ni katika kuhakikisha kwamba mchezo wa soka unaendelea kupata mafanikio zaidi nchini.
TFF imeanza mkutano wake huo wa mwaka baada ya kutanguliwa na kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika juzi katika Hotel ya Hans Poppe kunakoendelea pia mkutano huo.
Soka Ligi Kuu NBC kutumia VAR
Ligi Kuu NBC kutumia VAR
Read also