Korea Kusini
Mshambuliaji wa Norwich City, Hwang Ui-jo (pichani) kutoka Korea Kusini amesimamishwa na chama cha soka cha nchi yake akichunguzwa kwa kashfa ya kumrekodi picha za utupu mpenzi wake wa zamani.
Hwang Ui-jo, 31, anatuhumiwa kumrekodi mpenzi wake huyo wakati wakifanya ngono kwa kutumia simu ya mkononi na baadaye kutawanya picha hizo kwenye mitandao ya kijamii.
Mchezaji huyo ambaye juzi Jumanne alicheza mechi ya Norwich dhidi ya Watford na kufunga bao huku timu yake ikilala kwa mabao 4-2, alikana tuhuma zinazomkabili.
Hwang Ui-jo anaichezea Norwich kwa mkopo akitokea Nottingham Forest, wakati uchunguzi wa vyombo vya usalama ukiendelea, hakuwa tayari kuzungumza lolote na waandishi wa habari.
Mapema mwezi huu, Hwang Ui-jo aliiwakilisha Korea Kusini katika mechi mbili za kufuzu Kombe la Dunia na kufunga bao la penalti katika mechi na Singapore na ilitarajiwa awemo kwenye kikosi cha timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Asia zitakazofanyika Qatar kuanzia Januari 12 mwakani.
Kamati ya nidhamu ya Chama cha Soka Korea Kusini (KFA) imetangaza kumsimamisha mchezaji huyo wakati polisi wakiendela na uchunguzi hivyo huenda Januari mwakani asiwemo kwenye kikosi cha timu yake ya taifa.
Kocha wa timu ya Korea Kusini, Jurgen Klinsmann, akizungumzia sakata hilo alisema kwamba anaelewa mazingira ya tukio zima na ataheshimu uamuzi utakaofikiwa.
Kimataifa Picha za ngono zamponza mchezaji Korea Kusini
Picha za ngono zamponza mchezaji Korea Kusini
Related posts
Read also