Madrid, Hispania
Kipa wa zamani wa Man United, David de Gea inadaiwa amekataa ofa ya kuungana nyota mwenzake wa zamani wa Man United Cristiano Ronaldo katika klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia.
De Gea, kipa wa Hispania amekuwa bila timu tangu akatae kuongeza mkataba Man United na habari zaidi zinadai kwamba Al Nassr wapo tayari kumlipa Pauni 500,000 kwa wiki lakini amekataa ofa hiyo.
Kipa huyo pia amekuwa akihusishwa na mipango ya kuungana na nyota wa zamani wa Barcelona, Lionel Messi katika klabu ya Inter Miami FC ya Marekani lakini hadi sasa hajaonesha utayari wowote wa kuichangamkia ofa hiyo.
De Gea alizua hali ya mshangao baada ya kukaa kimya wakati akisubiriwa kusaini mkataba mpya Man United lakini hadi ilipofika majira ya kiangazi mwaka jana aligoma moja kwa moja kwa kilichodaiwa kuwa alitaka maslahi zaidi.
Tangu hapo amekuwa akihusishwa na mipango ya kujiunga na klabu mbalimbali za barani Ulaya lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika na haishangazi kuona habari zake zimehamia katika klabu za Marekani na Saudi Arabia.
Kimataifa De Gea akataa ofa ya Saudi Arabia
De Gea akataa ofa ya Saudi Arabia
Read also