Casablanca , Morocco
Al Ahly ya Misri imetwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya sare ya bao 1-1 na Wydad Casablanca ya Morocco na hivyo kuweka rekodi ya kubeba mara 11 taji la michuano hiyo mikubwa ya klabu barani Afrika.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumapili hii usiku, Ahly walipata bao la kusawazisha katika dakika ya 78 lililofungwa kwa kichwa na Mohamed Abdelmoneim kutokana na mpira wa kona uliopigwa na Ali Maaloul.
Kwa matokeo hayo, Ahly imefanikiwa kulibeba taji hilo kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2 baada ya ushindi wa mechi ya kwanza ya fainali wa mabao 2-1, mechi iliyopigwa mjini Cairo, Misri.
Ushindi umekuwa tukio kubwa la kuwafuta machozi Ahly ambao msimu uliopita walishindwa kutamba mbele ya vigogo hao wa Morocco walipolala kwa mabao 2-0 katika mechi moja ya fainali iliyopigwa mjini Casablanca.
Kabla ya Abdelmoneim kusawazishia bao, Wydad walikuwa mbele kwa bao ambalo pia lilifungwa na Yahya Attiat katika dakika ya 28, bao ambalo lingetosha kuwapa Wydad taji na kuwafanya waweke rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutoka Morocco kubeba taji hilo mara mbili mfululizo.
Hata hivyo mwisho wa siku walikuwa ni Ahly waliotoka uwanjani na shangwe wakineemeka na bao la Abdelmoneim na hivyo kuweka rekodi ya kulibeba taji hilo lenye hadhi barani Afrika kwa mara 11.
Kimataifa Al Ahly baba wa Afrika
Al Ahly baba wa Afrika
Read also