London, England
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amesema kocha mkongwe wa timu hiyo, Arsene Wenger amechagua wakati sahihi wa kurudi kwenye Uwanja wa Emirates kuishuhudia timu hiyo ikiwa katika mbio sahihi za kulisaka taji la Ligi Kuu England (EPL).
Arsenal jana Jumatatu ilitoka uwanjani kishujaa na ushindi wa mabao 3-1 katika mechi ya EPL baada ya kuwa nyuma kwa bao moja, ilikuja juu katika kipindi cha pili na kusawazisha bao hilo kabla ya kuongeza mabao mengine mawili.
Wenger ndiye aliyekuwa kocha wa mwisho wa Arsenal kubeba taji la Ligi Kuu England kabla ya kung’atuka mwaka 2018 lakini tangu ang’atuke jana alirudi kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa Emirates na kuishuhudia timu hiyo ikitokana na ushindi.
“Uwapo wake ni lazima liwe jambo kubwa mno linalohusika moja kwa moja na klabu hii ya soka, kwa hiyo tunamshukuru sana kwa alichokifanya kwa sababu kina maana kubwa kwa kila mtu katika klabu hii,” alisema Arteta.
“Ni matumaini yetu kwamba atakuwa tayari kuendelea kuwa hapa kwa muda mwingi zaidi kwa sababu ni mtu anayetoa hamasa kubwa,” alisema Arteta.
Katika mechi hiyo, West Ham ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na Said Benrahman katika dakika ya 27 baada ya Jarrod Bowen kukwatulia katika eneo la ndani ya 18 na William Saliba.
Bao hilo lilionekana kuwavuruga mashabiki wa Arsenal hadi walipotulizwa katika dakika ya 53 kwa bao lililofungwa na Bukayo saka aliyeinasa pasi ya Martin Odergaard.
Dakika tano baadaye, Gabriel Martinelli aliifungia Arsenal bao la pili ambaye aliupiga mpira ambao ilionekana kama anapiga krosi lakini ukajaa wavuni na kumshinda kipa wa West Ham, Lukasz Fabianski ambaye ni kipa wa zamani wa Arsenal. Bao la tatu la Arsenal lilifungwa na Eddie Nketiah katika dakika ya 69 kwa pasi ya Ødegaard.
Matokeo hayo yanaifanya Arsenal izidi kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa EPL kwa tofauti ya pointi nane ikiwa mbele ya Newcastle inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 32 katika mechi 16 wakati Arsenal imecheza mechi 15.
Matokeo ya mechi nyingine za EPL zilizochezwa Jumatatu ni kama ifuatavyo…
Brentford 2-2 Tottenham
Crystal Palace 0-3 Fulham
Everton 1-2 Wolves
Leicester 0-3 Newcastle
Southampton 1-3 Brighton
Aston Villa 1-3 Liverpool
Kimataifa Arteta ampa tano Wenger
Arteta ampa tano Wenger
Related posts
Read also