Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Simba Queens, Charles Lukula amesema kuwa wapo tayari kuivaa Determine Girls ya Liberia kesho wakiwa na lengo la kupata la kupata ushindi wa kwanza kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ya Wanawake.
Katika ligi hiyo inayoendelea nchini Morocco, Simba ilifungwa bao 1-0 kwenye mechi yake ya kwanza dhidi ya wenyeji AS FAR kwenye mchezo wa Kundi A.
Lukula ameeleza kuwa maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na wachezaji wake wote wapo fiti kiafya na kiakili na wanaingia kwenye mchezo huo lengo lao likiwa ni kupata ushindi.
Alisema baada ya kupoteza mchezo uliopita wachezaji wake walichukizwa kutokana na kiwango kizuri walichokionesha na mwisho kupoteza lakini amewataka kusahau hilo na kuweka nguvu na akili zao kwenye mchezo ulio mbele yao dhidi ya Determine.
“Ni kweli tulianza vibaya mashindano lakini nina imani kubwa na timu yangu lakini pia nina imani tutafuzu kucheza nusu fainali kwa kushinda mechi zote mbili zinazotukabili tukianza dhidi ya Determine Girls na Green Buffaloes, uwezo huo tunao,” alisema Lukula raia wa Uganda.
Kocha huyo ameeleza kuwa sababu ya matumaini hayo ni kutokana na kuziona timu hizo zikicheza kwenye mchezo wao wa ufunguzi na kubaini mapungufu mengi ukilinganisha na timu yake ambayo imeonesha ubora wa juu kwenye mchezo wao wa kwanza.
Determine ambao watamaliza kibarua chao cha mechi za makundi dhidi ya AS FAR kwenye mechi yao ya kwanza walipoteza kwa kubugizwa mabao 4-0 na Buffaloes.
Soka Simba Queens hakuna kukata tamaa
Simba Queens hakuna kukata tamaa
Related posts
Read also