London, England
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amewataka wachezaji wake kuhakikisha wanapata pointi muhimu katika mechi yao na PSV Eindhoven leo Alhamisi usiku na hatimaye kushika usukani wa Kundi A katika michuano ya Europa Ligi.
Arsenal au The Gunners tayari imefuzu hatua ya mtoano ya michuano hiyo baada ya kushinda mechi zake zote nne hadi sasa lakini anachotaka Arteta sasa ni timu hiyo kuepuka kucheza play-off dhidi ya timu mojawapo itakayotolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
“Wiki iliyopita tulipiga hatua ya kwanza ambayo ni kufuzu raundi inayofuata, tunahitaji kushinda Alhamisi kwa sababu tunataka kumaliza tukiwa wa kwanza,” alisema Arteta. Barcelona, Ajax na Atletico Madrid ni miongoni mwa timu zilizoangukia Europa Ligi baada ya kukwama kwenye Ligi ya Mabingwa.
“Mashindano yanakuwa magumu zaidi na zaidi, inaonekana kama vile raundi inayofuata itakuwa na ushindani mkubwa, na ndio maana kumaliza wa kwanza katika kundi na kuepuka mechi nyingine mbili ni jambo muhimu kwetu,” alisema Arteta.
Mechi za Europa Ligi leo Alhamisi ni kama ifuatavyo…
PSV Eindhoven v Arsenal
Man Utd v Sheriff Tiraspol
FC Zürich v Bodø/Glimt
AEK Larnaca v Dynamo Kyiv
Fenerbahçe v Rennes
Ludogorets v Real Betis
Union Berlin v Sporting Braga
Malmö FF v Union Saint-Gilloise
Lazio v FC Midtjylland
HJK Helsinki v Roma
Omonia Nicosia v Real Sociedad
SK Sturm Graz v Feyenoord
Kimataifa Arteta ataka pointi PSV
Arteta ataka pointi PSV
Related posts
Read also