Milan, Italia
Beki wa zamani wa timu ya Taifa ya Italia na klabu ya Real Madrid, Fabio Cannavaro amepata kibarua cha ukocha katika klabu ya Benevento ya Serie B Italia, hicho kikiwa kibarua chake cha kwanza Ulaya.
Cannavaro ambaye ndiye aliyekuwa nahodha wa timu ya Italia iliyobeba Kombe la Dunia mwaka 2006 alistaafu rasmi soka mwaka 2011 na kujikita katika kazi ya ukocha ambayo ameifanyakatika nchi za China na Saudi Arabia na baadaye kuinoa timu ya Taifa ya China mwaka 2019 kazi ambayo hata hivyo aliifanya kwa wiki sita tu.
Katika kazi ya ukocha mara ya mwisho, Cannavaro alikuwa akiinoa klabu ya Guangzhou FC ya China ambayo aliachana nayo Oktoba 2021, hiyo ikiwa ni kazi yake ya mwisho kabla ya kupata kibarua kipya na klabu ya Benevento.
Kazi kubwa ya Cannavaro katika timu ya Benevento ni kuhakikisha anarudisha katika Ligi Kuu Italia yaani Serie A baada ya kushuka katika msimu wa 2020-21 na kwa sasa inashika nafasi ya 13 katika Serie B ikiwa na pointi saba katika mechi sita.
Kabla ya kustaafu soka, Cannavaro enzi zake za soka la ushindani, mbali na Real Madrid pia ametamba na timu za Parma, Juventus na Inter Milan akiwa mmoja wa mabeki mahiri wa kati na mwaka 2006 alitwaa tuzo, Ballon d’Or.
Kimataifa Cannavaro kuinoa timu Serie B
Cannavaro kuinoa timu Serie B
Related posts
Read also