London, England
Nahodha wa zamani wa England, David Beckham amelazimika kupanga gfoleni kwa saa 12 ili kupata nafasi ya kumuona na kutoa heshima za mwisho kwa Malkia Elizabeth 11 wa Uingereza.
Beckham mwenye umri wa miaka 47 alikuwa miongoni mwa kundi kubwa la watu waliojitokeza kwa ajili ya kupita mbele ya jeneza la Malkia lililowekwa Westminster Hall ambapo staa huyo wa zamani wa klabu za Manchester United na Real Madrid alionekana akifuta machozi.
“Hii ni siku ya kipekee, kukumbushana na kusikiliza habari tofauti tofauti ambazo watu wanazijua,” alisema Beckham ambaye mwaka 2003 alipewa tuzo maalum ya heshima au OBE na Malkia huyo kutokana na mchango wake kwenye soka.
Akikumbukia tuzo hiyo Beckham alisema, “katika kupewa OBE niliambatana na bibi na babu yangu ambao kwa hakika ni wapenzi wa familia ya kifalme na kama ilivyo ada nilikuwa na mke wangu pia, kufika kwao, kupewa heshima na pia kukutana na Malkia na kuulizwa maswali, kuzungumza, nilikuwa mwenye bahati ya kufikia hatua hiyo katika maisha yangu, kuwa karibu na Malkia.”
“Hii ni siku ya huzuni lakini pia ni siku ya kukumbuka kumbukumbu za kipekee aliyotuachia Malkia, wakati wote tulipokuwa pale na mavazi yale tuliimbia Mungu amlinde Malkia, hilo ni jambo lenye maana kubwa kwangu,” alisema.
Beckham alikuwa katika foleni ndefu Ijumaa na kundi kubwa la watu kuanzia saa 8 usiku na wakati wote huo walikuwa wakinywa kahawa na vitafunwa vidogo vidogo ambapo alisema, “sote tulitaka kuwa hapa pamoja, tunataka kuwa na kumbukumbu ya kufurahia maisha ya Malkia na nafikiri hili ni jambo ambalo tunahitaji kulifanya pamoja.”
“Kwa wakati wote siku ya leo ni ngumu, ni ngumu kwa taifa, ngumu kwa kila mtu duniani kote, kwa sababu nafikiri kila mtu analihisi hili na fikra zetu zipo pamoja na familia na kila mmoja aliye hapa, nilidhani kwa kuja saa 8 kungekuwa kidogo kumetulia lakini nilikosea, haikuwa hivyo,” alisema Beckham akizungumzia wingi wa watu na jinsi alivyolazimika kupanga foleni.
Kimataifa Beckham apanga foleni saa 12 kumuaga Malkia
Beckham apanga foleni saa 12 kumuaga Malkia
Related posts
Read also