London, England
Vigogo wa Ligi Kuu England, Man City na Chelsea zinatarajia kuumana katika mechi za raundi ya tatu ya fainali za Carabao Cup zitakazopigwa kati ya Novemba 8 na 10 mwaka huu.
Mechi hiyo inaweza kuwa nafasi nyingine muhimu kwa Raheem Sterling wa Chelsea kudhihirisha ubora wake dhidi ya timu yake ya zamani ya Man City ambayo ililazimika kumuuza katika klabu ya Chelsea licha ya uwezo aliokuwa nao kwa kile kilichodaiwa kuwa ni shauku ya mchezaji huyo kutaka nafasi ya mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza.
Man City ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, katika mechi hiyo watakuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Etihad dhidi ya timu ambayo msimu uliopita ilifikia hatua ya fainali ya michuano hiyo lakini ikashindwa kubeba taji.
Mbali na Man City na Chelsea, timu nyingine za Ligi Kuu England zitakazokutana katika hatua hiyo ni pamoja na Man United itakayovaana na Aston Villa wakati Tottenham itakuwa na kibarua dhidi ya Nottingham Forest na Arsenal itatoana jasho na Brighton.
Ratiba kamili ya mechi hizo ni kama ifuatavyo…
Leicester v Newport County
West Ham v Blackburn
Wolves v Leeds
Nottingham Forest v Tottenham
Man United v Aston Villa
Bournemouth v Everton
Liverpool v Derby
Burnley v Crawley
Bristol City v Lincoln
Man City v Chelsea
Stevenage v Charlton
MK Dons v Morecambe
Newcastle v Crystal Palace
Southampton v Sheffield Wed
Arsenal v Brighton
Brentford v Gillingham
Kimataifa Chelsea, Man City kuvaana Carabao Cup
Chelsea, Man City kuvaana Carabao Cup
Related posts
Read also