Na mwandishi wetu
Mtanange wa fainali ya Kombe la Azam (ASFC) baina ya Coastal Union dhidi ya Yanga, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha keshokutwa, utaamuliwa na mwamuzi Ahmed Arajiga wa Manyara.
Hii ni mara ya pili, Arajiga anaamua mchezo wa pili wa Yanga wa FA mfululizo baada ya kuamua mechi yao iliyopita ya nusu fainali dhidi ya Simba na Yanga kushinda kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Pia kwa Arajiga inakuwa fainali yake ya pili mfululizo ya kombe hilo baada ya msimu uliopita kuchezesha fainali baina ya Simba na Yanga iliyopigwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma huku Simba ikiibuka kidedea kwa ushindi wa bao 1-0.
Waamuzi wasaidizi wa mchezo huo wa kufunga rasmi msimu wa soka Tanzania Bara 2021/22 ni Frank Komba na Janeth Balama huku mwamuzi wa akiba akiwa Radhani Kayoko.
Soka Refa ni Arajiga tena
Refa ni Arajiga tena
Related posts
Read also