London, England
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ametangazwa na Chama cha Makocha wa Soka England kuwa ndiye kocha bora wa msimu wa Ligi Kuu England wakati, kocha wa timu ya wanawake ya Chelsea, Emma Hayes naye ametwaa tuzo kama hiyo kwa upande wa wanawake.
Klopp ndiye aliyeiongoza Liverpool kutwaa taji la FA na lile la Ligi huku Jumamosi ijayo akiwania taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid wakati, Emma ameiongoza timu ya wanawake ya Chelsea kutwaa taji la wanawake kwa mara tatu mfululizo pamoja na taji la nne la FA.
Baada ya kutangazwa kutwaa tuzo hiyo, Benitez alisema kwamba ni heshima kubwa kwake hasa kwa kuwa ameipata tuzo kutokana na kura zilizopigwa na watu wake hivyo inabaki kuwa tuzo yenye umuhimu ambayo mtu anaweza kuipata.
Klopp (54) msimu huu alikuwa na malengo ya kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutwaa mataji manne lakini Jumapili iliyopita alilikosa taji la Ligi Kuu England lililobebwa na Man City.
Kocha huyo kutoka Ujerumani kwa sasa anasubiriwa kwa hamu kuona kama Jumamosi ijayo atabeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na hivyo kufikisha mataji matatu kwa msimu badala ya manne aliyotarajia awali.
Kimataifa Klopp kocha bora wa msimu
Klopp kocha bora wa msimu
Related posts
Read also