Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars, Kim Polsen ametaja kikosi cha wachezaji 27 akiwemo Himid Mao ambaye hajajumuishwa kwenye kikosi hicho kwa muda mrefu. Stars inajiandaa kwa ajili ya mechi za kuwania kushiriki michuano ya Afcon 2023.
Mbali na Himid anayekipiga Ghazł El Mahalla ya Misri, wengine ni makipa Aishi Manula wa Simba, Metacha Mnata (Polisi Tanzania) na Abutwalib Mshery (Yanga). Mabeki ni Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Kennedy Juma (wote Simba), Kibwana Shomari, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto (wote Yanga). Abdallah Kheri wa Azam, Nickson Kibabage (KMC), Haji Mnoga (Weymouth) na Novatus Dismas (Beitar Tel Aviv).
Wengine waliotajwa ni Mzamiru Yassin (Simba), Aziz Andabwile (Mbeya City), Simon Msuva (Wydad), Kelvin John (Genk), Feisal Salum (Yanga), Ben Starkie (Spalding), Farid Mussa (Yanga), Abdul Seleman (Coastal Union), Reliants Lusajo (Namungo), Kibu Denis (Simba), George Mpole (Geita Gold), Ibrahim Joshua (Tusker), Salum Abubakar (Yanga) na Mbwana Samatta (Antwerp).
Kikosi hicho kitaingia kambini hivi karibuni kwa ajili ya mechi hizo za kufuzu Afcon zinazotarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni, mwaka huu.
Stars ambayo mara ya mwisho kushiriki Afcon ilikuwa mwaka 2019 nchini Misri kabla ya kutolewa mapema kwenye hatua ya makundi, safari hii imepangwa Kundi F lenye timu za Algeria, Uganda na Niger.
Bingwa mtetezi, timu ya taifa ya Senegal itaanza harakati za kutetea kombe lake katika kundi L ambalo linashirikisha timu za Jamhuri ya Benin, Rwanda na Msumbiji wakati mwenyeji wa michuano, Ivory Coast imepangwa Kundi H dhidi ya timu za Zambia, Comoro na Lesotho.
Soka Kim aita 27 Stars, yumo Himid Mao
Kim aita 27 Stars, yumo Himid Mao
Related posts
Read also