Green Sports - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 18 Aug 2026 18:27:22 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Green Sports - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Fifa yalaumiwa kwa usaliti https://www.greensports.co.tz/2026/08/18/fifa-yalaumiwa-kwa-usaliti/ https://www.greensports.co.tz/2026/08/18/fifa-yalaumiwa-kwa-usaliti/#respond Tue, 18 Aug 2026 18:27:21 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14834 Nyon, UswiziShirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) na rais wake, Gianni Infantino wamelaumiwa kwa usaliti kupitia barua ya wazi ya mashirikisho ya soka Ulaya (Uefa), Marekani Kusini (Concacaf) na Asia.Barua hiyo ambayo imesainiwa marais na makatibu wakuu wa mashirikisho hayo matatu, imeeleza kuwa hoja ya hivi karibuni yenye utata inayohusisha Fifa Foward Enterprise (FFE) msingi […]

The post Fifa yalaumiwa kwa usaliti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Rais wa Fifa, Gianni Infantino

Nyon, Uswizi
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) na rais wake, Gianni Infantino wamelaumiwa kwa usaliti kupitia barua ya wazi ya mashirikisho ya soka Ulaya (Uefa), Marekani Kusini (Concacaf) na Asia.
Barua hiyo ambayo imesainiwa marais na makatibu wakuu wa mashirikisho hayo matatu, imeeleza kuwa hoja ya hivi karibuni yenye utata inayohusisha Fifa Foward Enterprise (FFE) msingi wake ni kuhusu hadhi ya soka na hadhi ya waliochaguliwa kuongoza mchezo huo.
Kwa mantiki hiyo FFE ilitaka kuwe na taasisi mpya itakayoundwa kusimamia haki za kibiashara na mauzo ya tiketi katika mashindano yote yanayosimamiwa na Fifa zikiwamo fainali za Kombe la Dunia ambapo asilimia 21 ingeuzwa kwa kampuni binafsi.
Mpango huo ulivunjwa baada ya kuibuka shutuma kutoka mashirikisho ya soka yakiongozwa na Uefa, shirisho ambalo lilitishia kususia mashindano yote ya soka yanayoandaliwa na Fifa.

“Inapotokea uaminifu ukavunjwa kwa kufanyika ulaghai, pale mtu mmoja anapoamua kujiweka juu ya ushirika uliomuamini na kumpa madaraka, hapo uaminifu unakuwa umewekwa kando,” ilieleza sehemu ya barua hiyo.


“Uongozi wa soka si jambo analomiliki mtu, si suala linaloshikiliwa na mtu au kulazimisha kushika madaraka badala yake ni wajibu wa kuzihudumia mamlaka za familia ya soka ambazo zimekuamini,” ilieleza barua hiyo.
Barua hiyo hata hivyo haikumtaja moja kwa moja Rais wa Fifa, Gianni Infantino lakini kilichopo ni kwamba mlengwa mkuu wa hoja hizo ni kiongozi huyo ambaye ni kama vile anatakiwa ajiuzulu.
Barua ya mashirikisho hayo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Fifa kutoa taarifa kwenye vyombo vya habari ikielezea kuhusu inachokiona kuwa ni juhudi za kififisha hadhi ya shirikisho hilo na Infantino.

The post Fifa yalaumiwa kwa usaliti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/08/18/fifa-yalaumiwa-kwa-usaliti/feed/ 0
Tamasha Yanga Day laingia doa https://www.greensports.co.tz/2026/08/18/tamasha-yanga-day-laingia-doa/ https://www.greensports.co.tz/2026/08/18/tamasha-yanga-day-laingia-doa/#respond Tue, 18 Aug 2026 18:23:37 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14831 Na mwandishi wetuTamasha ya Yanga Day limeingia doa baada ya timu hiyo kuchapwa mabao 2-1 na timu ya Aigles du Congo ya DR Congo katika mechi ya kirafiki iliyochezwa Jumapili Agosti 8, 2026 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.Katika mchezo huo uliotanguliwa na shamrashamra za kuwatambulisha wachezaji wapya wa Yanga kwa ajili ya msimu […]

The post Tamasha Yanga Day laingia doa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Tamasha ya Yanga Day limeingia doa baada ya timu hiyo kuchapwa mabao 2-1 na timu ya Aigles du Congo ya DR Congo katika mechi ya kirafiki iliyochezwa Jumapili Agosti 8, 2026 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo uliotanguliwa na shamrashamra za kuwatambulisha wachezaji wapya wa Yanga kwa ajili ya msimu mpya wa 2026-26, Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na mchezaji wao mpya, Peter Shalulile.
Shalulile alifunga bao hilo katika dakika ya 27 kwa mkwaju wa penalti lakini iliwachukua Aigles dakika 10 kupata bao la kusawazisha lililofungwa na Talasy Tonny na kuzifanya timu ziende mapumziko zikiwa sare.
Aigles waliandika bao la pili katika dakika ya 65, mfungaji kwa mara nyingine akiwa Tony na kuifanya timu yake itoke uwanjani na ushindi.
Mchezo huo umelipa benchi la ufundi la Yanga nafasi nzuri ya kukifanyia tathmini kikosi hicho kipya kabla ya kuanza mbio za kulitetea taji la Ligi Kuu NBC msimu wa 2026-27.
Yanga itaanza kuufungua msimu mpya kwa kuumana na mahasimu wao Simba katika mechi ya Ngao ya Jamii itakayopigwa Jumatano Agosti 12, 2026 kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.

The post Tamasha Yanga Day laingia doa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/08/18/tamasha-yanga-day-laingia-doa/feed/ 0
Baada ya kumkosa Vini Jr, Arteta ajipanga upya https://www.greensports.co.tz/2026/08/16/baada-ya-kumkosa-vini-jr-arteta-ajipanga-upya/ https://www.greensports.co.tz/2026/08/16/baada-ya-kumkosa-vini-jr-arteta-ajipanga-upya/#respond Sun, 16 Aug 2026 19:43:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14828 London, EnglandKocha wa Arsenal, Mikel Arteta amesema ataendelea kusajili wachezaji ili kukifanya kikosi chake kiwe bora baada ya kumkosa Vinicius Junior ‘Vini Jr’ aliyekubali kuongeza mkataba Real Madrid.Baada ya kuwapo uvumi kuhusu Arsenal kumsajili Vini Jr kutoka Real Madrid, hali ilibadilika kwa mchezaji huyo kukubali ofa nono ya miaka sita na sasa Arsenal wameamua kuhamishia […]

The post Baada ya kumkosa Vini Jr, Arteta ajipanga upya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amesema ataendelea kusajili wachezaji ili kukifanya kikosi chake kiwe bora baada ya kumkosa Vinicius Junior ‘Vini Jr’ aliyekubali kuongeza mkataba Real Madrid.
Baada ya kuwapo uvumi kuhusu Arsenal kumsajili Vini Jr kutoka Real Madrid, hali ilibadilika kwa mchezaji huyo kukubali ofa nono ya miaka sita na sasa Arsenal wameamua kuhamishia nguvu zao kwingineko.
Arteta aliulizwa na waandishi wa habari baada ya mechi ya kirafiki dhidi ya Borussia Dortmund Jumapili iliyopita iwapo mashabiki watarajie ongezeko la wachezaji, kocha huyo alisema hicho ndicho wanachotaka kukifanya.

“Ni lazima awe mchezaji sahihi katika soko ili kukifanya kikosi chetu kiwe bora zaidi, tunaliangalia hilo kwa sasa,” alisema Arteta.


Kabla ya Arsenal kufungwa mabao 3-2 na Borussia Dortmund kwenye Uwanja wa Emirates, siku hiyo hiyo walimtambulisha Bruno Guimarães kutoka Newcastle, aliyesajiliwa kwa Pauni 75 milioni.
Habari za ndani hata hivyo zinadai kwamba bado Arteta anataka mchezaji wa hadhi ya juu wa nafasi ya winga ya kushoto, matarajio ya awali yalikuwa kwa Vinicius kwa imani kuwa angekuwa na mchango mkubwa.
Arsenal pia inadaiwa kusaka mchezaji mahiri wa nafasi ya ulinzi wakati kukiwa na habari kwamba William Saliba anatarajia kuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu akisumbuliwa na matatizo ya mgongo.
Arteta alikiri timu yake kufanya makosa yaliyosababisha wafungwe mabao matatu jambo ambalo alisema wanatakiwa kulifanya kazi ili kuhakikisha wanakuwa bora kwa kuanzia na wachezaji waliopo.

The post Baada ya kumkosa Vini Jr, Arteta ajipanga upya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/08/16/baada-ya-kumkosa-vini-jr-arteta-ajipanga-upya/feed/ 0
Polisi Kenya watibua sherehe miaka 90 Simba https://www.greensports.co.tz/2026/08/09/polisi-kenya-watibua-sherehe-miaka-90-simba/ https://www.greensports.co.tz/2026/08/09/polisi-kenya-watibua-sherehe-miaka-90-simba/#respond Sun, 09 Aug 2026 19:12:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14825 Na mwandishi wetuSherehe za Simba Day zilizoandamana na kumbukumbu ya miaka 90 tangu kuanzishwa kwa klabu ya Simba zimeingia doa baada ya timu hiyo kuchapwa bao 1-0 na Polisi Kenya, mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.Simba na Polisi Kenya zimeumana Jumamosi Agosti 8, 2026, mechi iliyotanguliwa na sherehe hizo sambamba na utambulisho […]

The post Polisi Kenya watibua sherehe miaka 90 Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Sherehe za Simba Day zilizoandamana na kumbukumbu ya miaka 90 tangu kuanzishwa kwa klabu ya Simba zimeingia doa baada ya timu hiyo kuchapwa bao 1-0 na Polisi Kenya, mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Simba na Polisi Kenya zimeumana Jumamosi Agosti 8, 2026, mechi iliyotanguliwa na sherehe hizo sambamba na utambulisho wa wachezaji wa timu hiyo kwa ajili ya msimu mpya wa 2026-27.
Sherehe hizo zilipambwa na burudani ya muziki iliyofanywa na wasanii mbalimbali wakiongozwa na Ali Kiba ambapo mashabiki pia walimshuhudia mnyama Simba akiingizwa kunogesha tukio hilo.
Aliyepeleka kilio Simba alikuwa ni mshambuliaji wa zamani wa Singida Black Stars, Elvis Rupia aliyefunga bao hilo pekee katika dakika ya 90 ya mchezo huo.
Simba licha ya kufungwa bao hilo pekee lakini waliweza kukonga nyoyo za mashabiki waliofurika uwanjani hapo kwa kucheza soka safi na la kuvutia.
Timu hiyo ilitengeneza nafasi kadhaa za kufunga ambazo walishindwa kuzitumia huku wapinzani wao kutoka Kenya wakicheza kwa tahadhari kubwa hadi walipopata bao hilo pekee.
Kabla ya kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu NBC, Simba itapata nafasi nyingine ya kupima ubora wa kikosi chake kwa kuumana na mahasimu wao Yanga katika mechi ya Ngao ya Jamii itakayopigwa Agosti 12, 2026 kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.
Sherehe za Simba Day hufanyika kila mwaka tangu kuasisiwa mwaka 2009 na aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Hassan Dalali na katibu wake, Mwina Kaduguda.
Kwa mwaka huu sherehe za Simba Day zimenogeshwa na tukio la kumbukumbu ya miaka 90 tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo mwaka 1936.

The post Polisi Kenya watibua sherehe miaka 90 Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/08/09/polisi-kenya-watibua-sherehe-miaka-90-simba/feed/ 0
Viní Jr aongeza miaka 6 Real Madrid https://www.greensports.co.tz/2026/08/09/vini-jr-aongeza-miaka-6-real-madrid/ https://www.greensports.co.tz/2026/08/09/vini-jr-aongeza-miaka-6-real-madrid/#respond Sun, 09 Aug 2026 19:10:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14823 Madrid, HispaniaMshambuliaji Vinícius Junior ‘Vini Jr’ wa Real Madrid hatimaye amevunja ukimya kwa kukubali ofa mpya inayoandamana na mkataba wa miaka sita itakayomfanya awe na klabu hiyo hadi mwaka 2032.Klabu ya Real Madrid imethibitisha hilo Alhamisi Agosti 6, 2026 na hivyo kumaliza uvumi wa siku za hivi karibuni kuhusu hatma ya Vini Jr ambaye pia […]

The post Viní Jr aongeza miaka 6 Real Madrid first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Mshambuliaji Vinícius Junior ‘Vini Jr’ wa Real Madrid hatimaye amevunja ukimya kwa kukubali ofa mpya inayoandamana na mkataba wa miaka sita itakayomfanya awe na klabu hiyo hadi mwaka 2032.
Klabu ya Real Madrid imethibitisha hilo Alhamisi Agosti 6, 2026 na hivyo kumaliza uvumi wa siku za hivi karibuni kuhusu hatma ya Vini Jr ambaye pia huichezea timu ya taifa ya Brazil.
Mazungumzo baina ya wawakilishi wa Vini na mabosi wa Real Madrid yalikwenda vizuri na inadaiwa kuwa makubaliano yamefikiwa baada ya maslahi ya mchezaji huyo kuboreshwa.
Kabla ya hapo mazungumzo yaliyoanza takriban mwaka mmoja uliopita baina ya pande mbili husika yalikuwa yakikwama na kuibua hofu kuhusu hatma ya Vini Jr na Real Madrid.
Mkataba wa Vini Jr na Real Madrid unafikia ukomo Juni 2027 na kukaibuka habari zilizodai kwamba mchezaji huyo hatoongeza mkataba na tayari alianza kuhusishwa na klabu kadhaa lakini hatimaye amekubali kuongeza mkataba Real Madrid hadi 2032.

“Real Madrid na Vinícius tumekubaliana kuongeza mkataba wa mchezaji wetu, atakuwa katika klabu hii hadi Juni 2032,” ilieleza taarifa ya klabu hiyo.


Vini Jr alijiunga na Real Madrid Julai 2018 wakati huo akiwa na umri wa miaka 18 na katika misimu yake minane na klabu hiyo hadi sasa amebeba mataji mbalimbali.
Awali kulikuwa na habari kuwa Real Madrid ilikuwa tayari kumuuza Vini Jr kama makubaliano yasingefikiwa na moja ya klabu iliyokuwa ikimtaka kwa hali na mali ni Arsenal ya England.
Viní Jr tayari ameshaanza mazoezi katika uwanja wa mazoezi wa Valdebebas unaomilikiwa na Real Madrid baada ya mapumziko.
Mara ya mwisho alionekana akiiwakilisha Brazil kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 kabla ya timu hiyo kutolewa na Norway katika hatua ya robo fainali.

The post Viní Jr aongeza miaka 6 Real Madrid first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/08/09/vini-jr-aongeza-miaka-6-real-madrid/feed/ 0
Hersi apewa miaka mingine minne Yanga https://www.greensports.co.tz/2026/08/09/hersi-apewa-miaka-mingine-minne-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2026/08/09/hersi-apewa-miaka-mingine-minne-yanga/#respond Sun, 09 Aug 2026 19:05:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14820 Na mwandishi wetuInjinia Hersi Said ataendelea kuiongoza klabu ya Yanga kwa kipindi kingine cha miaka minne baada ya kupita bila kupingwa katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam Jumapili, Agosti 2, 2026.Ushindi huo umekuja katika mkutano mkuu wa uchaguzi wa klabu hiyo ambapo kiongozi huyo hakuwa na mpinzani kama ilivyokuwa kwa […]

The post Hersi apewa miaka mingine minne Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Injinia Hersi Said ataendelea kuiongoza klabu ya Yanga kwa kipindi kingine cha miaka minne baada ya kupita bila kupingwa katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam Jumapili, Agosti 2, 2026.
Ushindi huo umekuja katika mkutano mkuu wa uchaguzi wa klabu hiyo ambapo kiongozi huyo hakuwa na mpinzani kama ilivyokuwa kwa makamu wake, Arafat Haji ambao wataendelea kuiongoza klabu hiyo.
Katika nafasi za wajumbe watano wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo, walioshinda ni Munir Seleman, Alexander Ngai, Yanga Makaga, Julius Koi na Fahd Afif.
Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Hersi aliwataka wanachama wa klabu hiyo kuvunja kambi zilizotokana na makundi ya uchaguzi na kuwa kitu kimoja.
Kwa upande wa wagombea walioshindwa katika uchaguzi huo, Hersi aliwataka kutoyapokea matokeo hayo kwa chuki kwa kuwa wao bado ni wanachama wa Yanga.
Hersi aliwapongeza wagombea ambao wamefanikiwa kushinda katika nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji wakiwamo wawili aliosema kuwa ni wapya na wengine watatu wamebaki.
“Wagombea waliokosa nafasi nao ni washindi licha ya kwamba kura hazikutosha, hawatakiwi kuwa maadui wa klabu yetu badala yake wanapaswa kuwa sehemu ya klabu yao,” alisema Hersi.
Katika mkutano huo, Hersi pia alipata nafasi ya kuwaeleza wanachama mafanikio ya uongozi wake tangu akabidhiwe jukumu hilo takriban miaka minne iliyopita.

The post Hersi apewa miaka mingine minne Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/08/09/hersi-apewa-miaka-mingine-minne-yanga/feed/ 0
Hispania bingwa Kombe la Dunia 2026 https://www.greensports.co.tz/2026/07/20/hispania-bingwa-kombe-la-dunia-2026/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/20/hispania-bingwa-kombe-la-dunia-2026/#respond Sun, 19 Jul 2026 23:05:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14816 New York, MarekaniFerran Torres ameibuka shujaa baada ya kufunga bao pekee na kuiwezesha Hispania kutoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Argentina na kutwaa Kombe la Dunia 2026.Iliwachukua Hispania dakika 106 kupata bao hilo licha ya kuutawala mchezo na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Argentina lakini mashambulizi hayo hayakuweza kuzaa bao kwa dakika 90 […]

The post Hispania bingwa Kombe la Dunia 2026 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Ferran Torres ameibuka shujaa baada ya kufunga bao pekee na kuiwezesha Hispania kutoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Argentina na kutwaa Kombe la Dunia 2026.
Iliwachukua Hispania dakika 106 kupata bao hilo licha ya kuutawala mchezo na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Argentina lakini mashambulizi hayo hayakuweza kuzaa bao kwa dakika 90 za kawaida.
Kikwazo kikubwa kwa Hispania alikuwa kipa wa Argentina, Emilio Martinez ambaye aliokoa michomo kadhaa ya Hispania hadi kumaliza dakika 90 timu hizo zikiwa hazijafungana ndipo zilipoongezwa dakika 30.
Katika dakika 30 za nyongeza Hispania waliendelea kulisakama lango la Argentina huku Argentina wakitumia muda mwingi kujihami kabla hawajaadhibiwa dakika ya 106 na Torres aliyefunga bao kwa shuti kali la mguu wa kushoto.
Bao hilo lilianzia kwa mpira mrefu uliopigwa na Lamine Yamal na kumkuta Nico William ambaye alimuunganishia Torres pasi ya kichwa na Torres kufumua shuti lililomshinda Martinez.
Baada ya kuingia bao hilo, Argentina waliokuwa wamezidiwa kila idara, waliamka na kuanza mashambulizi wakiongozwa na Lionel Messi na kuibua hali ya hofu kwa Hispania.
Messi ambaye alishindwa kuonesha umahiri wake kwa kipindi kirefu, bao la Hispania ni kama lilimpa nguvu ya kuongoza mashambulizi yaliyozaa kona mbili za haraka kwenye lango la Hispania.
Ukiachana na mashambulizi hayo yaliyopamba moto baada ya Argentina kufungwa, kwa dakika zote 120, timu hiyo ilifanikiwa kupiga mashuti mawili tu ya maana langoni mwa Hispania.
Dalili za Hispania kutoka na ushindi zilianza kuonekana mapema kwa namna walivyotawala mchezo na kulisakama lango la Argentina waliokuwa na kazi ya kujihami huku wakishindwa kutengeneza mashambulizi ya maana.
Kasi ya mashambulizi ya Hispania kwenye lango la Argentina ilianza kuonekana mapema dakika za 4 na 5, Lamine Yamal alionesha umahiri lakini mashuti yake mawili yaliishia mikononi mwa kipa Martinez.
Hispania kwa mara nyingine dakika ya 38 ilifanya shambulizi langoni mwa Argentina lakini shuti la chinichini la mguu wa kushoto lililopigwa na Mikel Oyarzabal lilidakwa na kipa Martinez.
Hispania pia mara kadhaa ilifanya mashambulizi yaliyotokea upande wa kushoto kwa beki Cucurella lakini krosi za beki huyo ziliokolewa au kutoka nje ya lango.
MAmbo yalizidi kuwaharibikia Argentina baada ya nyota wao Enzo Fernandes kulimwa kadi ya pili ya njano kwa kucheza rafu na hivyo kutoka uwanjani akiwaacha wenzake 10 kupambana katika dakika 30 za nyongeza.
Hispania ambao mara ya mwisho walilibeba Kombe la Dunia mwaka 2010 katika fainali zilizofanyika nchini Afrika Kusini, pia ndio mabingwa wa Kombe la Ulaya 2024 au Euro 2024.
Fainali za Kombe la Dunia zilianza kutimua vumbi Juni 11, 2026 katika nchi za Canada, Mexico na kuhitimishwa Jumapili, Julai 19, 2026 nchini Marekani kwa mechi iliyopigwa mjini New York kwenye Uwanja wa New Jersey.

The post Hispania bingwa Kombe la Dunia 2026 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/20/hispania-bingwa-kombe-la-dunia-2026/feed/ 0
Kelvin Nashon rasmi mali ya Simba https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/kelvin-nashon-rasmi-mali-ya-simba/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/kelvin-nashon-rasmi-mali-ya-simba/#respond Sun, 19 Jul 2026 14:56:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14813 Na mwandishi wetuBaada ya kuwapo uvumi kuhusu Kelvin Nashon kutua Simba, hatimaye klabu hyo imemtangaza rasmi kiungo huyo kuwa mchezaji wao mpya atakayeitumikia timu hiyo kuanzia msimu mpya wa 2026-27.Taarifa hiyo rasmi imepatikana leo Jumapili Julai 19, 2026 kwenye mitandao ya kijamii ya klabu hiyo ikiambatana na picha ya kumkaribisha kiungo huyo fundi kutoka Pamba […]

The post Kelvin Nashon rasmi mali ya Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Baada ya kuwapo uvumi kuhusu Kelvin Nashon kutua Simba, hatimaye klabu hyo imemtangaza rasmi kiungo huyo kuwa mchezaji wao mpya atakayeitumikia timu hiyo kuanzia msimu mpya wa 2026-27.
Taarifa hiyo rasmi imepatikana leo Jumapili Julai 19, 2026 kwenye mitandao ya kijamii ya klabu hiyo ikiambatana na picha ya kumkaribisha kiungo huyo fundi kutoka Pamba Jiji.
Habari za Kelvin kujiunga na Simba zimekuwapo kwa miezi kadhaa lakini hazikuwa zimethibitishwa na klabu hiyo na hivyo sasa ni rasmi kuanzia msimu ujao nyota huyo ambaye pia amewahi kuichezea Singida Black Stars atavaa jezi ya Simba.
Habari za Simba kumtaka kiungo huyo ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, zilianza kusikika wakati akiwa Singida Black Stars kabla ya kwenda Pamba Jiji, Januari 2025.
Simba ambayo imemaliza Ligi Kuu NBC msimu ulioisha wa 2025-26 ikiwa nafasi ya pili, inaendelea kuimarisha kikosi chake ikiacha baadhi ya wachezaji na kusajili wapya kwa ajili ya msimu mpya wa ligi hiyo na michuano ya kimataifa.
Azam, Yanga nazo zasajili
Wakati Simba ikikamilisha usajili huo Azam FC nao wameendelea kukiimarisha kikosi chao kwa kumsajili winga Henoc Nolia kutoka FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Mitadao ya Azam kuanzia Jumamosi Julai 18, 2026 imepambwa na picha za mchezaji huyo mpya ambaye ataongeza nguvu katika kikosi cha timu hiyo iliyomaliza nafasi ya tatu katika Ligi Kuu NBC msimu wa 2025-26.
Nao mabingwa watetezi wa Ligi Kuu NBC, Yanga wametangaza kumsajili mshambuliaji Juma Issa Abushiri maarufu Chuga Boy kutoka Fountain Gate FC.
Chuga ndiye mchezaji wa kwanza kutambulishwa na Yanga kwa ajili ya kukiongezea nguvu kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya msimu mpya wa 2026-27.

The post Kelvin Nashon rasmi mali ya Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/kelvin-nashon-rasmi-mali-ya-simba/feed/ 0
England yashika nafasi ya tatu https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/england-yashika-nafasi-ya-tatu/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/england-yashika-nafasi-ya-tatu/#respond Sun, 19 Jul 2026 14:53:40 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14810 Miami, MarekaniEngland imeshika nafasi ya tatu kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 ikiilaza Ufaransa mabao 6-4 huku Jude Bellingham akiweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa timu hiyo kufunga mabao saba katika moja ya Kombe la Dunia.Timu hizo ziliumana katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu Jumamosi Julai 18, 2026 huku mechi ya […]

The post England yashika nafasi ya tatu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Miami, Marekani
England imeshika nafasi ya tatu kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 ikiilaza Ufaransa mabao 6-4 huku Jude Bellingham akiweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa timu hiyo kufunga mabao saba katika moja ya Kombe la Dunia.
Timu hizo ziliumana katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu Jumamosi Julai 18, 2026 huku mechi ya fainali kati ya Hispania na Argentina ikisubiriwa kupigwa Jumapili Julai 19, 2026.
Bellingham ambaye pia ni kiungo wa Real Madrid, awali alifungana na nahodha na mshambuliaji wa England, Harry Kane aliyefunga mabao sita katika fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.
Rekodi kama hiyo ya mabao sita kabla ya hapo ilikuwa ikishikiliwa na Garry Lineker aliyeifungia England idadi mabao kama hiyo ya mabao kwenye fainali za Kombe la Dunia 1986 nchini Mexico.
Katika mechi dhidi ya Ufaransa, Bellingham, 23, aliingizwa uwanjani dakika ya 79 na kufunga bao lililotokana na shambulizi la kushtukiza.
Dakika 12 kabla ya hapo alikuwa afunge bao kwa mkwaju wa penalti lakini akaamua kumpa nafasi hiyo Bukayo Saka ambaye hakumuangusha, aliitumia vyema penalti hiyo kuipatia England bao.
Saka hata hivyo baada ya mechi alisema kwamba ni Bellingham ndiye aliyemwambia aende akapige mpira huo wa penalti ili apate hat trick (mabao matatu).
Katika mechi hiyo mbali na Bellingham, mabao mengine ya England yalifungwa na Declan Rice dakika ya tatu, Konsa dakika ya 18 na Saka ambaye alifunga dakika za 37, 45 na 87.
Mabao ya Ufaransa yalifungwa na Kylian Mbappe aliyefunga mawili dakika za 48 na 66 wakati mengine mawili yalifungwa na Barcola dakika ya 54 na Dembele dakika ya 90.

The post England yashika nafasi ya tatu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/england-yashika-nafasi-ya-tatu/feed/ 0
Chasambi aachwa Simba https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/chasambi-aachwa-simba/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/chasambi-aachwa-simba/#respond Sun, 19 Jul 2026 11:34:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14807 Na mwandishi wetuKlabu ya soka ya Simba imetangaza kuachanana winga wake Ladack Chasambi ambaye sasa ni rasmi hatokuwa na timu hiyo kwa msimu ujao wa 2026-27.Taarifa iliyopatikana Jumamosi Julai 18, 2026 kwenye vyanzo vya habari vya klabu hiyo, imemtaja mchezaji huyo kuwa mmoja wa wachezaji ambao wamepewa nafasi ya kutafuta maisha nje ya Simba.Chasambi alijiunga […]

The post Chasambi aachwa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya soka ya Simba imetangaza kuachanana winga wake Ladack Chasambi ambaye sasa ni rasmi hatokuwa na timu hiyo kwa msimu ujao wa 2026-27.
Taarifa iliyopatikana Jumamosi Julai 18, 2026 kwenye vyanzo vya habari vya klabu hiyo, imemtaja mchezaji huyo kuwa mmoja wa wachezaji ambao wamepewa nafasi ya kutafuta maisha nje ya Simba.
Chasambi alijiunga na Simba Januari 2024 akitokea Mtibwa Sugar ambapo alipandishwa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo baada ya kuonesha uwezo wake kwenye timu ya vijana kabla ya Simba kuvutiwa naye.
Alisajiliwa na Simba wakati huo ikiwa chini ya kocha Abdelhak Benchikha akitajwa kuwa mmoja wa wachezaji waliopewa matumaini makubwa ya kutamba kutokana na uwezo alioanza kuuonesha.
Hali hata hivyo imekuwa tofauti kwa mchezaji huyo ambaye hatimaye Simba imetangaza rasmi kuachana naye.
Chasambi sasa anaungana na mshambuliaji wa timu hiyo, Jonathan Sowah ambaye naye alitangaza kuachwa baada ya kuichezea timu hiyo kwa msimu mmoja tu akitokea Singida Black Stars.
Mchezaji mwingine ambaye Simba imetangaza kuachana naye hivi karibuni ni kiungo mkongwe, Muzamir Yassin ambaye amekuwa na timu hiyo akicheza kwa mafanikio kwa takriban miaka 10.

The post Chasambi aachwa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/chasambi-aachwa-simba/feed/ 0