PSG - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 08 May 2024 06:24:19 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg PSG - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mbappe ajibebesha lawama PSG ikilala 1-0 https://www.greensports.co.tz/2024/05/08/mbappe-ajibebesha-lawama-psg-ikilala-1-0/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/08/mbappe-ajibebesha-lawama-psg-ikilala-1-0/#respond Wed, 08 May 2024 06:24:18 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10892 Paris, UfaransaMshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe amesema kushindwa kwa timu yake kufuzu hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kulala kwa bao 1-0 mbele ya Borussia Dortmund, sababu ni kupoteza nafasi zikiwamo alizopoteza yeye.PSG ikiwa nyumbani katika jiji la Paris, jana Jumanne ililala kwa bao 1-0 na hivyo kutolewa kwa jumla ya […]

The post Mbappe ajibebesha lawama PSG ikilala 1-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Paris, Ufaransa
Mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe amesema kushindwa kwa timu yake kufuzu hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kulala kwa bao 1-0 mbele ya Borussia Dortmund, sababu ni kupoteza nafasi zikiwamo alizopoteza yeye.
PSG ikiwa nyumbani katika jiji la Paris, jana Jumanne ililala kwa bao 1-0 na hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 2-0 baada ya kulala kwa bao 1-0 katika mechi ya nusu fainali ya kwanza.
Kwa matokeo hayo, Dortmund sasa inasubiri kucheza mechi ya fainali kwenye dimba la Wembley na mshindi wa mechi nyingine ya nusu fainali kati ya Real Madrid na Bayern Munich leo Jumatano.
Akizungumza baada ya matokeo hayo, Mbappe alisema kwamba katika mechi hiyo alijaribu kadri alivyoweza kuisaidia timu yake lakini hapo hapo alikiri kushindwa kufanya hivyo kiasi cha kutosha.
“Tunapozungumzia kuwa sahihi katika eneo la boksi, nafikiri mimi hapo ndiye mlengwa, mimi ni mtu ambaye ni lazima nifunge mabao na niwe makini, mambo yanapokuwa mazuri nabeba sifa zote na inapokuwa tofauti nabeba lawama, hilo si tatizo,” alisema Mbappe.
Akifafanua zaidi Mbappe alisema mtu wa kwanza ambaye ilikuwa lazima afunge ni yeye na kwamba kilichojitokeza ndivyo maisha yalivyo na sasa ni lazima yeye na wenzake waangalie mbele.
Mchezaji huyo ambaye anahusishwa na mipango ya kujiunga na Real Madrid alisema kwamba PSG si kwamba haikuwa na bahati bali haikuwa katika ubora kiasi cha kutosha.
PSG ambao walifanya mashambulizi kadhaa yakiwamo mashuti yaliyogonga mwamba, jambo ambalo Mbappe alisema linaonesha jinsi ambavyo hawakuwa vizuri na kwa upande wa Dortmund alisema hana uhakika kama timu hiyo ilikuwa bora zaidi yao.

“Sipendi kuzungumzia suala la kutokuwa na bahati, unapokuwa vizuri mashuti hayawezi kugonga mwamba, yanaingia nyavuni, leo (jana) hatukuwa vizuri sisi washambuliaji,” alisema Mbappe.


Bao lililoibeba Dortmund lilipatikana mapema kipindi cha pili mfungaji akiwa ni Mats Hummels na baada ya hapo timu hiyo ilifanya kazi nzuri kumdhibiti Mbappe ambaye huenda hiyo ikawa mechi yake ya mwisho ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na jezi ya PSG.

Mbappe hata hivyo alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu kujiunga na Real Madrid aliishia kukunja uso na kuondoka.
Naye kocha wa PSG, Luis Enrique aliwapongeza Dortmund kwa ushindi na kusema kwamba kilichoikuta timu yake kinasikitisha hasa kwa namna ambavyo walicheza vizuri na kufanya mashambulizi ya kutosha.
“Inasikitisha unapopoteza mchezo hasa kwa namna hii, tumegonga mwamba wa goli mara sita, tumepiga mashuti 31 lakini hatukuweza kufunga goli, inaonekana kama ni jambo gumu kuamini,” alisema Enrique.
Dortmund wakifanikiwa kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu watakuwa wanafanya hivyo kwa mara ya kwanza tangu kufanya hivyo mara ya mwisho mwaka 1997.

The post Mbappe ajibebesha lawama PSG ikilala 1-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/08/mbappe-ajibebesha-lawama-psg-ikilala-1-0/feed/ 0
Mbappe apewa jukumu la ulinzi PSG ikiivaa Dortmund https://www.greensports.co.tz/2024/05/07/mbappe-apewa-jukumu-la-ulinzi-psg/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/07/mbappe-apewa-jukumu-la-ulinzi-psg/#respond Tue, 07 May 2024 06:27:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10869 Paris, UfaransaKocha wa PSG, Luis Enrique amemtaka mshambuliaji wake Kylian Mbappé kufanya kazi ya ulinzi katika mechi ya nusu fainali ya pili dhidi ya Borussia Dortmund leo Jumanne ili kubadili matokeo baada ya kulala kwa bao 1-0 katika mechi ya kwanza.Enrique alikuwa akijibu swali aliloulizwa kuhusu nini anachoweza kufanya Mbappe ili kuipatia timu hiyo ushindi […]

The post Mbappe apewa jukumu la ulinzi PSG ikiivaa Dortmund first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Kylian Mbappe

Paris, Ufaransa
Kocha wa PSG, Luis Enrique amemtaka mshambuliaji wake Kylian Mbappé kufanya kazi ya ulinzi katika mechi ya nusu fainali ya pili dhidi ya Borussia Dortmund leo Jumanne ili kubadili matokeo baada ya kulala kwa bao 1-0 katika mechi ya kwanza.
Enrique alikuwa akijibu swali aliloulizwa kuhusu nini anachoweza kufanya Mbappe ili kuipatia timu hiyo ushindi ambapo kocha huyo alisema mshambuliaji huyo nyota anahitaji kutoa mchango wake katika eneo lote la uwanja.
“Sisi ni timu, tunawataka washambuliaji kusaidia kuhakikisha mipira inafika mara chache kwenye eneo letu la ulinzi, kwa pamoja kila mmoja ana wajibu wa kutoa mchango wake, hata mchezaji nyota duniani anatakiwa kusaidia katika ulinzi,” alisema Enrique.
Enrique hata hivyo alisema kwamba ana matumaini ya timu yake kutoka na ushindi katika mechi hiyo na hatimaye kucheza fainali ya michuano hiyo mikubwa ya ngazi ya klabu barani Ulaya.
Kocha huyo pia alisema kwamba kitendo cha kuwa nyuma katika mechi ya kwanza si jambo ambalo linamfanya aogope badala yake anaamini timu yake ipo vizuri kimtazamo na kifikra kwa ajili ya mechi hiyo.

“Nafikiri unahitaji utulivu wa kifikra ili kukabiliana na jambo lolote katika taaluma yako au maisha yako binafsi, wakati wote jiandae mambo yanaweza kwenda vibaya kama ni lazima iwe hivyo na uwe tayari kubadili hali hiyo,” alisema Enrique.


Kwa upande wake kocha wa Dortmund, Edin Terzic alisema timu yake inahitaji kuboresha kiwango ilichokionesha katika mechi ya kwanza ili iweze kufuzu na hatimaye kusonga mbele na kucheza mechi ya fainali.

The post Mbappe apewa jukumu la ulinzi PSG ikiivaa Dortmund first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/07/mbappe-apewa-jukumu-la-ulinzi-psg/feed/ 0
Enrique aamini PSG itaizamisha Barca https://www.greensports.co.tz/2024/04/16/enrique-aamini-psg-itaizamisha-barca/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/16/enrique-aamini-psg-itaizamisha-barca/#respond Tue, 16 Apr 2024 07:19:31 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10621 Paris, UfaransaKocha wa PSG, Luis Enrique amesema anaamini timu yake inaweza kupindua meza na kuibuka na ushindi katika mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona itakayopigwa leo Jumanne.Katikam mechi ya kwanza iliyopigwa mjini Paris, Barca iliibuka na ushindi wa mabao 3-2, matokeo ambayo pia yaliifanya PSG ibaki na rekodi ya […]

The post Enrique aamini PSG itaizamisha Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Paris, Ufaransa
Kocha wa PSG, Luis Enrique amesema anaamini timu yake inaweza kupindua meza na kuibuka na ushindi katika mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona itakayopigwa leo Jumanne.
Katikam mechi ya kwanza iliyopigwa mjini Paris, Barca iliibuka na ushindi wa mabao 3-2, matokeo ambayo pia yaliifanya PSG ibaki na rekodi ya kucheza mechi 27 za mashindano yote bila kupoteza hata moja.
Enrique alikuwa kocha wa Barça mwaka 2017 na kufanikiwa kupindua meza baada ya kufungwa mabao 4-0 na PSG lakini katika mechi ya pili waliichapa PSG 6-1 na sasa kocha huyo anataka jambo hilo lijirudie akiwa kocha PSG.
“PSG haijawahi kupindua meza baada ya kufungwa katika mechi ya kwanza, lakini Jumanne ndio siku ya kufanya hivyo,” alisema Enrique katika mkutano na waandishi wa habari.
“Baada ya kupoteza mechi muhimu, baada ya mechi hiyo mambo yanakuwa magumu, ni mtego fulani, kunakuwa na ugumu kujiweka sawa kisaikolojia lakini jambo zuri katika soka ni kwamba baada ya hapo unakuwa na mechi nyingine dhidi ya mpinzani yule yule,” alisema Enrique.
Kabla ya mechi ya kwanza baina ya timu hizo, Enrique anakumbukwa kwa kusema kwamba analijua vyema soka la Barca kumzidi kocha wa sasa wa timu hiyo, Xavi Hernandez na msimamo wake utaendelea kuwa hivyo ingawa hiyo haimaanishi kwamba haheshimu kazi ya Xavi.
Kwa upande wake, Xavi yeye alisema kwamba anamuweka Enrique kwa ubora sawa na makocha wa kiwango cha juu kina Pep Guardiola na Luis Aragones na kwake kati ya makocha bora waliowahi kumfundisha.
Xavi ambaye leo ana faida ya kuwa nyumbani, aliwahi kucheza soka na Enrique wakiwa Barça na baadaye katika msimu wa 2014-15, Enrique alikuwa kocha wa Barca, Xavi akiwa mchezaji.
Mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya leo Jumanne
Barca v PSG
B Dortmund v Atl Madrid
Mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya kesho Jumatano
Bayern Munich v Arsenal
Man City v Real Madrid

The post Enrique aamini PSG itaizamisha Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/16/enrique-aamini-psg-itaizamisha-barca/feed/ 0
Mbappe aipeleka PSG robo fainali Ulaya https://www.greensports.co.tz/2024/03/06/mbappe-aipeleka-psg-robo-fainali-ulaya/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/06/mbappe-aipeleka-psg-robo-fainali-ulaya/#respond Wed, 06 Mar 2024 06:03:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10051 Madrid, HispaniaKocha wa PSG, Luis Enrique huenda akalazimika kufikiria upya uamuzi wake wa kutaka timu hiyo ianze mapema kujipanga bila ya Kylian Mbappe baada ya mshambuliaji huyo kufunga mabao mawili na kuiwezesha PSG kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.Enrique alitangaza mpango huo na kuanza kuufanyia kazi katika mechi mbili za Ligi 1 dhidi […]

The post Mbappe aipeleka PSG robo fainali Ulaya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Kylian Mbappe

Madrid, Hispania
Kocha wa PSG, Luis Enrique huenda akalazimika kufikiria upya uamuzi wake wa kutaka timu hiyo ianze mapema kujipanga bila ya Kylian Mbappe baada ya mshambuliaji huyo kufunga mabao mawili na kuiwezesha PSG kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Enrique alitangaza mpango huo na kuanza kuufanyia kazi katika mechi mbili za Ligi 1 dhidi ya Rennes na dhidi ya Monaco, alimuweka benchi Mbappe baada ya kucheza kwa dakika kadhaa na mechi zote hizo ziliisha kwa sare.
Mabao mawili ya Mbappe aliyofunga jana Jumanne usiku dhidi ya Real Sociedad yameifanya PSG kutoka uwanjani na ushindi wa 2-1 na kufuzu robo fainali kwa ushindi wa jumla wa 4-1, mabao hayo yanatosha kabisa kumfikirisha upya Enrique, bao pekee la Sociedad lilifungwa na Merino.
Si Enrique pekee, hata mabosi PSG nao wana kazi ya kutafakari kama ni sahihi kumuachia Mbappe aondoke licha ya ukweli kwamba mkataba wake unafikia ukomo mwishoni mwa msimu huu na habari zilizopo ni kwamba mazungumzo yake na Real Madrid yanakwenda vizuri.
Kutokana na juhudi hizo za Mbappe, PSG sasa wanasubiri hapo Machi 15 ili kumjua mpinzani wao katika mechi ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa ya klabu barani Ulaya..
Nayo Bayern Munich, timu ambayo imekuwa na msimu mbaya katika Ligi Kuu ya Ujerumani au Bundesliga, jana ilifanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuilaza Lazio mabao 3-0 na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1.
Katika mechi hiyo nyota ya nahodha wa England, Harry Kane iling’ara baada ya kutupia wavuni mabao mawili peke yake wakati bao la tatu likifungwa na Muller.
Matokeo ya mechi za jana Ligi ya Mabingwa Ulaya…
Bayern Munich 3-0 Lazio
Real Sociedad 1-2 PSG

The post Mbappe aipeleka PSG robo fainali Ulaya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/06/mbappe-aipeleka-psg-robo-fainali-ulaya/feed/ 0
Messi aitolea uvivu PSG https://www.greensports.co.tz/2023/09/23/messi-aitolea-uvivu-psg/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/23/messi-aitolea-uvivu-psg/#respond Sat, 23 Sep 2023 13:39:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7838 Miami, MaarekaniMshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi amesema alichukizwa kwa kutopewa heshima na klabu yake ya zamani wa PSG baada ya kubeba kombe la dunia wakati wachezaji wenzake wote wa Argentina walipewa heshima hiyo na klabu zao.Katika mechi ya fainali kati ya Argentina na Ufaransa, Messi alifunga mabao mawili na lingine la […]

The post Messi aitolea uvivu PSG first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Miami, Maarekani
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi amesema alichukizwa kwa kutopewa heshima na klabu yake ya zamani wa PSG baada ya kubeba kombe la dunia wakati wachezaji wenzake wote wa Argentina walipewa heshima hiyo na klabu zao.
Katika mechi ya fainali kati ya Argentina na Ufaransa, Messi alifunga mabao mawili na lingine la tatu kwenye mikwaju ya penalti na kuiwezesha Argentina kutoka na ushindi wa 4-2 na hatimaye kubeba Kombe la Dunia katika fainali zilizopigwa Qatar, Novemba na Desemba mwaka jana.
Akizungumzia hali ilivyokuwa baada ya ushindi huo aliporejea katika klabu yake Messi alisema, “mimi nilikuwa mchezaji pekee kati ya 25 ambaye sikupewa heshima na klabu.”
Messi katika hilo alifafanua, “inaeleweka, kwa sababu sisi (Argentina) wao (Ufaransa) hawakuweza kulitetea Kombe la Dunia.”
Katika usajili wa dirisha kubwa la kiangazi, mwezi Juni, Messi aliachana na PSG na alikuwa na wakati mgumu katika klabu hiyo na alikiri kwamba kulikuwa na tatizo kati yake na baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo katika misimu miwili aliyoichezea.
Alipoulizwa kama hakupenda kujiunga na PSG, Messi alisema, “Ilitokea kama ilivyokuwa, halikuwa jambo ambalo nililitarajia lakini wakati wote huwa nasema, kuna mambo hutokea kwa sababu, hata kama sikuwa vizuri pale lakini ilitokea kwamba nilikuwa bingwa wa dunia wakati nikiwa pale.”
Akiizungumzia klabu yake ya sasa ya Inter Miami FC ya Marekeni, Messi alisema kwamba anafurahia soka lake katika klabu hiyo.

“Napenda ninachokifanya, nafurahia kucheza na kwa sasa nacheza katika namna tofauti, na hii ndio sababu iliyonifanya nichukua uamuzi wa kuja Miami na si kuendelea na soka kwingineko, unapata uzoefu tofauti,” alisema Messi.


Kuhusu uwezekano wa kustaafu soka, Messi mwenye umri wa miaka 36 sasa alisema kwamba hafikirii jambo hilo na hajaufuta uwezekano wa kurudi nyumbani Argentina na kuichezea klabu yake ya zamani ya utotoni ya Newell’s Old Boys kabla ya kustaafu soka hasa baada ya kuwa tayari amebeba taji la dunia.

The post Messi aitolea uvivu PSG first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/23/messi-aitolea-uvivu-psg/feed/ 0
Mbappe aibeba PSG Ligi ya Mabingwa https://www.greensports.co.tz/2023/09/20/mbappe-aibeba-psg-ligi-ya-mabingwa/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/20/mbappe-aibeba-psg-ligi-ya-mabingwa/#respond Wed, 20 Sep 2023 08:03:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7798 Paris, UfaransaMshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe ameuanza vizuri msimu mpya wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kufunga bao wakati timu yake ikiilaza Borussia Dortmund mabao 2-0 na kuibua matumaini mapya.PSG katika miaka ya karibuni ikiwa na wachezaji mastaa Lionel Messi, Neymar na wengineo imekuwa ikishindwa kufurukuta katika michuano hiyo na badala yake kuishia kutamba katika […]

The post Mbappe aibeba PSG Ligi ya Mabingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Paris, Ufaransa
Mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe ameuanza vizuri msimu mpya wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kufunga bao wakati timu yake ikiilaza Borussia Dortmund mabao 2-0 na kuibua matumaini mapya.
PSG katika miaka ya karibuni ikiwa na wachezaji mastaa Lionel Messi, Neymar na wengineo imekuwa ikishindwa kufurukuta katika michuano hiyo na badala yake kuishia kutamba katika Ligi 1 ya Ufaransa.
Messi na Neymar wameihama timu hiyo, Messi akitimkia nchini Marekani katika klabu ya Inter Miami wakati Neymar amejiunga na Al Hilal ya Saudi Arabia.
Katika mechi na Dortmund iliyopigwa jana, Mbappe alifunga bao kwa mkwaju wa penalti dakika ya 49 baada ya Nicklas Sule kuunawa mpira uliopigwa na mshambuliaji huyo na mwamuzi kuamuru ipigwe penalti.
Bao la pili la PSG lilipatikana katika dakika ya 58 mfungaji akiwa ni beki Achraf Hakimi baada ya kushirikiana vizuri na kiungo Vitinha aliyemuunganishia pasi ya kisigino.
PSG waliutawala vyema mchezo huo tangu mwanzo lakini juhudi zao zilikatishwa tamaa na Dortmund hususan katika kipindi cha kwanza.
Ushindi huo unakuwa wa kwanza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kocha mpya wa timu hiyo Luis Enrique ambaye pamoja na mambo mengine ana jukumu zito la kuipa mafanikio hasa kwenye ligi hiyo ya klabu barani Ulaya ambayo ni kubwa na maarufu duniani kote.
Matokeo ya mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya za jana Jumanne ni kama ifuatavyo…
AC Milan 0-0 Newcastle
Feyenoord 2-0 Celtic
Lazio 1-1 Atl Madrid
PSG 2-0 B Dortmund
Man City 3-1 Red Star Belgrade
Barcelona 5-0 Royal Antwerp
Young Boys 1-3 RB Leipzig
Shakhtar Donetsk 1-3 FC Porto

The post Mbappe aibeba PSG Ligi ya Mabingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/20/mbappe-aibeba-psg-ligi-ya-mabingwa/feed/ 0
Rais PSG amjibu Neymar https://www.greensports.co.tz/2023/09/08/rais-psg-amjibu-neymar/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/08/rais-psg-amjibu-neymar/#respond Fri, 08 Sep 2023 13:36:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7697 Paris, UfaransaRais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi (pichani) amewajibu aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo, Neymar na aliyekuwa mkurugenzi wa michezo, Leonardo akisema kwamba PSG kwa sasa ina umoja ambao haujawahi kutokea.Neymar hivi karibuni alisema kwamba alikuwa katika wakati mgumu akiwa PSG pamoja na mchezaji mwenzake, Lionel Messi ambao katika baadhi ya mechi walijikuta wakizomewa na baadhi […]

The post Rais PSG amjibu Neymar first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Paris, Ufaransa
Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi (pichani) amewajibu aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo, Neymar na aliyekuwa mkurugenzi wa michezo, Leonardo akisema kwamba PSG kwa sasa ina umoja ambao haujawahi kutokea.
Neymar hivi karibuni alisema kwamba alikuwa katika wakati mgumu akiwa PSG pamoja na mchezaji mwenzake, Lionel Messi ambao katika baadhi ya mechi walijikuta wakizomewa na baadhi ya mashabiki wa timu hiyo.
Leonardo naye aliwahi kunukuliwa akiushutumu uongozi wa PSG akisema kwamba Neymar, Messi na Kylian Mbappe walikosa kuungwa mkono na kuthaminiwa ili wawe katika mazingira mazuri ya kuipa timu hiyo ushindi.
Wakati Messi na Neymar wameihama timu hiyo, Mbappe ameendelea kubaki licha ya kuwapo utata kuhusu mkataba wake na Al-Khelaifi amempongeza mchezaji huyo ambaye pia ni nahodha wa timu ya Ufaransa pamoja na kuwajibu Neymar na Leonardo. “Kylian Mbappe ni mchezaji wa kipekee na mtu mzuri,” alisema Al-Khelaifi.

“Na timu ya PSG haijawahi kuwa katika umoja ndani na nje ya uwanja kama ilivyo sasa, hiki ni kitu ambacho tumekiona wikiendi hii katika mechi ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Lyon, tuna kocha mzuri (Luis Enrique) na mkurugenzi wa michezo, Luis Campos, na nina furaha kwa ari mpya iliyopo katika klabu,” alisema Al-Khelaifi.


Baada ya kuwakosa Messi aliyejiunga na Inter Miami FC ya Marekani na Neymar aliyetimkia Saudi Arabia, PSG ilianza Ligi 1 nchini Ufaransa kwa sare mbili kabla ya kuanza kuibuka na ushindi.
PSG ina kibarua kigumu kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwa kundi moja na timu za Newcastle, AC Milan na Borussia Dortmund ingawa Al-Khelaifi anaamini watakuwa na mafanikio katika fainali hizo msimu huu.
“Mwaka huu tupo katika muelekeo mpya, hatuangalii kwa sana matokeo badala yake tunaangalia kiwango na aina ya uchezaji wetu, kama tutaendelea hivyo, matokeo yatatufuata,” alisema Al-Khelaifi.
Al-Khelaifi pia alisema kuna watu wamesahau kwamba katika misimu minne iliyopita PSG ilifikia fainali na nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

The post Rais PSG amjibu Neymar first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/08/rais-psg-amjibu-neymar/feed/ 0
Kolo Muani akacha mazoezi, aitaka PSG https://www.greensports.co.tz/2023/08/30/kolo-muani-akacha-mazoezi-aitaka-psg/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/30/kolo-muani-akacha-mazoezi-aitaka-psg/#respond Wed, 30 Aug 2023 19:07:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7596 Frankfurt, UjerumaniMshambuliaji wa timu ya Eintracht Frankfurt, Randal Kolo Muani (pichani) amekwepa kufanya mazoezi ya timu hiyo leo Jumatano ikiwa ni mkakati wa kulazimisha kuhama ili ajiunge na PSG.Habari zaidi zinadai kwamba mshambuliaji huyo Mfaransa tayari yuko Paris, Ufaransa yalipo makao makuu ya klabu ya PSG ambayo inahaha kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.PSG imeondokewa na […]

The post Kolo Muani akacha mazoezi, aitaka PSG first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Frankfurt, Ujerumani
Mshambuliaji wa timu ya Eintracht Frankfurt, Randal Kolo Muani (pichani) amekwepa kufanya mazoezi ya timu hiyo leo Jumatano ikiwa ni mkakati wa kulazimisha kuhama ili ajiunge na PSG.
Habari zaidi zinadai kwamba mshambuliaji huyo Mfaransa tayari yuko Paris, Ufaransa yalipo makao makuu ya klabu ya PSG ambayo inahaha kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.
PSG imeondokewa na Lionel Messi aliyetimkia nchini Marekani katika klabu ya Inter Miami pamoja na Neymar ambaye hivi karibuni alijiunga na klabu tajiri ya Al Hilal ya Saudi Arabia.
Kolo Muani alishaweka wazi mpango wake huo mapema alipozungumza na chombo kimoja cha habari na kusema kwamba anataka kuhamia PSG.

“Mshambuliaji Randal Kolo Muani leo (Jumatano) ameuarifu uongozi wa klabu ya Eintracht Frankfurt kuwa hatofanya mazoezi ya mwisho kabla ya mechi ya Alhamisi ya Europa Conference Ligi dhidi ya Levski Sofia,” ilieleza taarifa ya Frankfurt.


“Amebainisha wazi azma yake ya kutaka kubadili klabu kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili Ijumaa usiku kuwa hiyo ndiyo sababu ya yeye kukosekana.”
Frankfurt bado inamhitaji mshambuliaji huyo ambaye alijiunga na timu hiyo akitokea Nantes ya Ufaransa na msimu uliopita ulikuwa na mafanikio kwake akifunga mabao 23 katika mechi 46 za mashindano tofauti na tayari ameuanza msimu huu na mabao matatu katika mechi nne.
Uamuzi wake wa kususia mazoezi umemkera mjumbe wa bodi ya klabu ya Frankfurt, Markus Krosche ambaye amesema kwamba huyu si Randal waliyemjua na wanayezijua vizuri tabia zake.
Mpango wa mchezaji huyo ambaye ameifungia timu ya taifa ya Ufaransa bao moja katika mechi tisa ukifanikiwa, akiwa PSG ataungana na nyota wenzake wa Ufaransa Kylian Mbappe na Ousmane Dembele.
Akiwa na timu ya Ufaransa mwaka jana kwenye fainali Kombe la Dunia, Kolo Muani anakumbukwa kutoa mchango mkubwa alipoingia katika mechi ya fainali dhidi ya Argentina, mechi ambayo iliisha kwa sare ya mabao 3-3 kabla ya Ufaransa kukwama kwenye mikwaju ya penalti.

The post Kolo Muani akacha mazoezi, aitaka PSG first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/30/kolo-muani-akacha-mazoezi-aitaka-psg/feed/ 0
Mbappe arejea mazoezini PSG https://www.greensports.co.tz/2023/08/13/mbappe-arejea-mazoezini-psg/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/13/mbappe-arejea-mazoezini-psg/#respond Sun, 13 Aug 2023 12:08:36 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7364 Paris, UfaransaMshambuliaji wa Paris St-Germain (PSG) ya Ufaransa, Kylian Mbappe (pichani) amerejea kwenye mazoezi ya kikosi cha kwanza na huenda hatua hiyo ikafuta rasmi mpango uliokuwa ukizungumzwa hivi karibuni wa kuihama PSG.Taarifa fupi ya PSG ilieleza kuwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amerudishwa kwenye kikosi cha kwanza baada ya mazungumzo mazuri yenye kujenga […]

The post Mbappe arejea mazoezini PSG first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Paris, Ufaransa
Mshambuliaji wa Paris St-Germain (PSG) ya Ufaransa, Kylian Mbappe (pichani) amerejea kwenye mazoezi ya kikosi cha kwanza na huenda hatua hiyo ikafuta rasmi mpango uliokuwa ukizungumzwa hivi karibuni wa kuihama PSG.
Taarifa fupi ya PSG ilieleza kuwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amerudishwa kwenye kikosi cha kwanza baada ya mazungumzo mazuri yenye kujenga na yaliyokua na mwelekeo chanya.
Mbappe aliondolewa kwenye mazoezi ya kikosi cha kwanza cha PSG na jana Jumamosi hakuwamo katika timu iliyocheza mechi ya kwanza ya Ligi 1 dhidi ya Lorient iliyomalizika kwa sare ya 0-0.
Kwa muda wote wa mechi hiyo, Mbappe alikuwa jukwaani akimshuhudia pia nyota mwenzake wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Ousmane Dembele akiiwakilisha PSG kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na timu hiyo kwa ada ya Pauni 43.5 milioni akitokea Barca.
Mbappe ameingia katika mgogoro na mabosi wa PSG kuhusu mkataba baada ya kugoma kusaini mkataba mpya wakati huu na awali aliachwa kwenye ziara ya PSG barani Asia iliyokuwa maalum kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi I wa 2023-24 ambao ulianza rasmi jana.
Katika siku za hivi karibuni amekuwa akihusishwa na mipango ya kujiunga na Real Madrid lakini jambo hilo halijakamilika hapo hapo Liverpool ilitangaza kuwa tayari kumsajili kwa mkopo, mpango ambao Mbappe aliukataa.
Mbappe ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa ya Ufaransa, pia alitakiwa na klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia ambayo iliruhusiwa kufanya naye mazungumzo kabla ya kutangaza kwamba ipo tayari kuweka rekodi ya dunia kwa kumsajili kwa Pauni 259 milioni lakini Mbappe pia alikataa.
Awali mabosi PSG walimtaka Mbappe achague moja kama ni kusani mkataba na timu hiyo wakati huu au kuondoka lakini Mbappe ambaye mkataba wake wa sasa na PSG unafikia ukomo Juni mwakani alishikilia msimamo wa kutotaka kusaini mkataba mpya lakini hataki kuondoka wakati huu.
Mbappe alijiunga na PSG mwaka 2017 akitokea Monaco kwa ada ya Pauni 165.7 milioni ambayo iliweka rekodi ya usajili katika klabu hiyo, hadi sasa ameweka rekodi ya kipekee akiifungia timu hiyo jumla ya mabao 212 katika mechi 260.

The post Mbappe arejea mazoezini PSG first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/13/mbappe-arejea-mazoezini-psg/feed/ 0
Dembele ahamia PSG https://www.greensports.co.tz/2023/08/02/dembele-ahamia-psg/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/02/dembele-ahamia-psg/#respond Wed, 02 Aug 2023 11:55:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7223 Las Vegas, MarekaniKocha wa Barcelona, Xavi Hernandez amesema kwamba mshambuliaji wa timu hiyo, Ousmane Dembele (pichani) anahamia PSG.Dembele mwenye umri wa miaka 26, alijiunga na Barca mwaka 2017 akitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani kwa ada ya Pauni 135 milioni na amefunga mabao 40 katika mechi 185 hadi sasa.Leo Jumatano Dembele alikuwa mmoja wa wachezaji wa […]

The post Dembele ahamia PSG first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Las Vegas, Marekani
Kocha wa Barcelona, Xavi Hernandez amesema kwamba mshambuliaji wa timu hiyo, Ousmane Dembele (pichani) anahamia PSG.
Dembele mwenye umri wa miaka 26, alijiunga na Barca mwaka 2017 akitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani kwa ada ya Pauni 135 milioni na amefunga mabao 40 katika mechi 185 hadi sasa.
Leo Jumatano Dembele alikuwa mmoja wa wachezaji wa akiba wa Barca katika mechi ya kirafiki dhidi ya AC Milan iliyopigwa mjini Las Vegas na Barca kutoka na ushindi wa bao 1-0 lakini mchezaji huyo hakucheza.
“Amesema kwamba hili ni wazo lake na ameamua kuondoka, ni uamuzi wake binafsi, napenda kuwa wazi katika hilo,” alisema Xavi.
“Ameamua kuwa muwazi, hilo ni wazo lake la kwenda Paris Saint Germain (PSG) kwamba ameitwa huko na sisi hapa hatuwezi kufanya lolote na ndio maana hakucheza hii leo,” alisema.

“Inaniuma mimi kwa sababu nafikiri tumekuwa tukimuangalia vizuri hapa ili awe mwenye furaha na kuwa nasi na kuendelea kuleta tofauti katika timu yetu,” aliongeza Xavi.


Mwaka jana, Dembele alisaini mkataba wa miaka miwili na Barca na kuweka rekodi ya kutoa asisti nyingi kwenye La Liga na Desemba mwaka jana alikuwamo kwenye timu ya Ufaransa iliyofikia hatua ya fainali ya Kombe la Dunia kabla ya kubwagwa na Argentina.
Msimu uliopita wa 2022-23 ambao Barca ilibeba taji la La Liga, Dembele alikosa sehemu kubwa ya nuus ya pili ya msimu huo kutokana na majeraha ya misuli yaliyokuwa yakimkabili.

The post Dembele ahamia PSG first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/02/dembele-ahamia-psg/feed/ 0