Maguire - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 04 May 2025 09:57:57 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Maguire - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Maguire: Mashabiki wanatudai https://www.greensports.co.tz/2025/05/03/maguire-mashabiki-wanatudai/ https://www.greensports.co.tz/2025/05/03/maguire-mashabiki-wanatudai/#respond Fri, 02 May 2025 21:07:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13375 Manchester, EnglandBeki wa Man United, Harry Maguire amesema wachezaji wa timu hiyo wanajiona wenye deni la kombe kwa mashabiki wao kutokana na imani waliyonayo baada ya kupitia katika msimu usio na mafanikio kwenye Ligi Kuu England (EPL).Kwa mwenendo wa ligi hiyo ulivyo kwa sasa ni wazi Man United itamaliza msimu huu ikiwa katika nafasi za […]

The post Maguire: Mashabiki wanatudai first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Manchester, England
Beki wa Man United, Harry Maguire amesema wachezaji wa timu hiyo wanajiona wenye deni la kombe kwa mashabiki wao kutokana na imani waliyonayo baada ya kupitia katika msimu usio na mafanikio kwenye Ligi Kuu England (EPL).
Kwa mwenendo wa ligi hiyo ulivyo kwa sasa ni wazi Man United itamaliza msimu huu ikiwa katika nafasi za katikati na hii ni mara ya kwanza tangu miaka ya 1990 ingawa kwa upande mwingine timu hiyo inaonekana kurudi katika ubora wao kwenye Europa Ligi.
Baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Athletic Bilbao ugenini Hispania jana Alhamisi, katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Europa Ligi, Maguire na wachezaji wenzake wapo katika mwelekeo mzuri wa kucheza mechi ya fainali ya ligi hiyo.
Mauire alisema hawana cha kuwaokoa katika msimu huu kwa sababu anafikiri umekuwa msimu wa kukatisha tamaa kwa kuwa wamekuwa na mechi nyingi walizopoteza na wameyumba kwa sana.

“Umekuwa msimu mgumu, wa kukatisha tamaa lakini ndio soka lilivyo, kunakuwa na mambo ya kukumbuka, ni mambo ya kutengeneza vitu vya kukumbukwa, ni suala la kushinda mataji na tuna nafasi kubwa ya kushinda taji,” alisema Maguire.


Maguire alisema kwamba hilo (taji) ni haki ambayo wanatakiwa kupewa mashabiki wa timu hiyo kwani ndicho kitu muhimu kwao.
Kocha wa Man United,r Ruben Amorim tangu aanze kuinoa timu hiyo ameshinda mechi saba kati ya tisa za Europa Ligi lakini katika EPL ameshinda mechi sita tu kati ya 23.
Wakati kocha huyo akijibebesha lawama kwa mwenendo mbaya kwenye ligi tangu ajiunge na timu hiyo Novemba mwaka jana, Maguire amewanyooshea kidole wachezaji wenzake kwa alichosema wana wajibu wa kuendana na mabadiliko ya makocha kutoka Erik ten Hag aliyetimuliwa na Amorim wa sasa.

The post Maguire: Mashabiki wanatudai first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/05/03/maguire-mashabiki-wanatudai/feed/ 0
Maguire asubiri mkataba mpya United https://www.greensports.co.tz/2024/12/17/maguire-asubiri-mkataba-mpya-united/ https://www.greensports.co.tz/2024/12/17/maguire-asubiri-mkataba-mpya-united/#respond Tue, 17 Dec 2024 18:54:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12431 Manchester, EnglandBeki wa kati wa Man United, Harry Maguire amesema hajakata tamaa ya kuongeza mkataba utakaombakisha katika klabu hiyo baada ya mazungumzo yenye matumaini kuhusu jambo hilo.Mkataba wa sasa wa Maguire na Man United unafikia ukomo mwishoni mwa msimu huu ingawa mkataba huo una kipengele kinachoipa Man United nafasi kumuongezea mkataba hadi 2026.Maguire amepitia kipindi […]

The post Maguire asubiri mkataba mpya United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Manchester, England
Beki wa kati wa Man United, Harry Maguire amesema hajakata tamaa ya kuongeza mkataba utakaombakisha katika klabu hiyo baada ya mazungumzo yenye matumaini kuhusu jambo hilo.
Mkataba wa sasa wa Maguire na Man United unafikia ukomo mwishoni mwa msimu huu ingawa mkataba huo una kipengele kinachoipa Man United nafasi kumuongezea mkataba hadi 2026.
Maguire amepitia kipindi kigumu Man United kutokana na anguko la kiwango chake na mwaka 2023 alikuwa katika mpango wa kujiunga na West Ham lakini jambo hilo halikufanikiwa.
Mambo yalionekana kuwa magumu kwa beki huyo baada ya kusajiliwa kwa Matthijs de Ligt na Leny Yoro na imani iliyokuwapo ni kwamba huo ulikuwa mwisho wake ndani ya kikosi hicho.
Maguire hata hivyo hakukata tamaa badala yake alitumia vyema kila nafasi aliyoipata kuonesha uwezo wake jambo lililotosha kumshawishi aliyekuwa kocha wake Eric ten Hag ambaye aliendelea kumuamini.
Katika mechi ya Jumapili dhidi ya Man City ambao ni mahasimu wao wa jiji la Manchester, nyota ya Maguire ilizidi kung’ara huku timu yake ikitoka na ushindi wa mabao 2-1.
Ushindi huo na kiwango chake cha hivi karibuni vimemfanya Maguire mwenye umri wa miaka 31 kuzidi kujipa matumaini ya kuongezewa mkataba Man United.
Mashabiki wengi walishangaa kumuona Maguire katika kikosi cha Man United kwenye mechi na Man City chini ya kocha wao mpya, Ruben Amorim ambaye ameteuliwa hivi karibuni kuchukua nafasi ya Ten Hag aliyetimuliwa.

The post Maguire asubiri mkataba mpya United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/12/17/maguire-asubiri-mkataba-mpya-united/feed/ 0
Maguire amsamehe mbunge wa Ghana aliyemdhihaki https://www.greensports.co.tz/2023/11/23/maguire-amsamehe-mbunge-wa-ghana-aliyemdhihaki/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/23/maguire-amsamehe-mbunge-wa-ghana-aliyemdhihaki/#respond Thu, 23 Nov 2023 19:38:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8609 Manchester, EnglandBeki wa Man United, Harry Maguire amekubali msamaha alioombwa na mbunge mmoja wa Ghana aliyedhihaki kiwango chake wakati akichangia usimamizi wa uchumi wa Ghana na kuufananisha na uchezaji mbovu wa mchezaji huyo.Akitumia mtandao wa Twitte au X, Maguire aliandika, “Tuonane Old Trafford,” kauli ambayo inaonesha kuwa mchezaji huyo amekubali yaishe.Mbunge huyo, Issac Adongo alikuwa […]

The post Maguire amsamehe mbunge wa Ghana aliyemdhihaki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Beki wa Man United, Harry Maguire amekubali msamaha alioombwa na mbunge mmoja wa Ghana aliyedhihaki kiwango chake wakati akichangia usimamizi wa uchumi wa Ghana na kuufananisha na uchezaji mbovu wa mchezaji huyo.
Akitumia mtandao wa Twitte au X, Maguire aliandika, “Tuonane Old Trafford,” kauli ambayo inaonesha kuwa mchezaji huyo amekubali yaishe.
Mbunge huyo, Issac Adongo alikuwa akichangia bajeti ya Ghana mwaka jana na kuufananisha usimamizi wa uchumi chini ya makamu rais wa Ghana, Mahamudu Bawumia na kiwango kibovu cha uchezaji cha Maguire.
Juzi Jumanne hata hivyo Adongo alisema kwamba anataka kusahihisha kauli yake hiyo na kumpongeza Maguire kwa namna ambavyo soka lake limebadilika na kuwa mchezaji tegemeo wa Man United.
Mbunge huyo hata hivyo hakubadili msimamo wake kuhusu lawama alizomtupia makamu wa rais kwa usimamizi mbovu wa uchumi.
Akifafanua zaidi mbunge huyo alisema kwamba alitumia mfano wa Maguire aliyekuwa chini ya kiwango msimu wa 2021-2022 ili kufikisha ujumbe wa kutoridhishwa na jinsi uchumi wa Ghana unavyosimamiwa.

“Kiwango cha Harry kilipoanza kuwa bora niliona analazimika kuombwa msamaha, nikiwa ni mpenzi wa soka ni muhimu kutambua mabadiliko yake,” alisema Adongo.


Bawumia kwa sasa ndiye kiongozi wa serikali ya Ghana anayesimamia uchumi wa nchi hiyo ambao unapitia katika kipindi kigumu nchi hiyo ikiandamwa na madeni yanayotokana na mkopo wa Shirika la Fedha Duniani (IMF).

The post Maguire amsamehe mbunge wa Ghana aliyemdhihaki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/23/maguire-amsamehe-mbunge-wa-ghana-aliyemdhihaki/feed/ 0
Maguire avuna matunda ya uvumilivu https://www.greensports.co.tz/2023/11/14/maguire-avuna-matunda-ya-uvumilivu/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/14/maguire-avuna-matunda-ya-uvumilivu/#respond Tue, 14 Nov 2023 06:18:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8441 Manchester, EnglandBeki wa Man United, Harry Maguire ambaye amekuwa akihaha kupata namba, amesema uamuzi wake wa kubaki katika klabu hiyo majira ya kiangazi umempa ushindi baada ya kurejea kikosi cha kwanza.Baada ya kuwa na wakati mgumu katika msimu wa kwanza chini ya kocha Erik ten Hag, Maguire alikuwa mbioni kujiunga na West Ham wakati wa […]

The post Maguire avuna matunda ya uvumilivu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Beki wa Man United, Harry Maguire ambaye amekuwa akihaha kupata namba, amesema uamuzi wake wa kubaki katika klabu hiyo majira ya kiangazi umempa ushindi baada ya kurejea kikosi cha kwanza.
Baada ya kuwa na wakati mgumu katika msimu wa kwanza chini ya kocha Erik ten Hag, Maguire alikuwa mbioni kujiunga na West Ham wakati wa dirisha la usajili lakini mwishowe aliamua kubaki Man United.
Msimu huu wa 2023-24 aliuanza akiwa benchi lakini katika mechi nane za michuano yote zilizopita, mchezaji huyo amekuwa akipata nafasi kikosi cha kwanza na hivyo anaamini alikuwa sahihi kuamua kubaki Man United.
“Nilicheza mechi chache mno msimu uliopita, 16 au 17 kwenye kikosi cha kwanza na nadhani nilicheza vizuri katika mechi nilizopata nafasi, japo sikucheza mechi nyingi kama ambavyo ningependa,” alisema Maguire.
“Nililazimika kuwa mvumilivu, nilipata nafasi mbili au tatu za kucheza msimu uliopita lakini nikajikuta katika majeruhi mara mbili, kwa hiyo sikuwa kwenye ile kasi na sikupata mechi mfululizo za kutosha ambazo ningeweza kuzitumia kumthibitishia kocha, nimepata nafasi hiyo sasa,” alisema Maguire.

“Hakika nafurahia soka langu na nafurahia hasa kuichezea hii klabu, nilikuwa tayari kubaki hapa na kupigania nafasi yangu na hapa tuna mabeki wa kati wenye hadhi ya kimataifa wanne au watano, ukweli ni kwamba ushindani wa namba ni mkubwa mno,” alisema Maguire.


Maguire kwa sasa ndiye beki wa bei mbaya zaidi duniani akiwa amesajiliwa Man United mwaka 2019 kutoka Leicester City kwa ada ya Pauni 80, na sasa ameanza kupata nafasi kikosi cha kwanza baada ya Martinez kuwa majeruhi wa muda mrefu.

The post Maguire avuna matunda ya uvumilivu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/14/maguire-avuna-matunda-ya-uvumilivu/feed/ 0
Maguire, Onana wageuka mashujaa https://www.greensports.co.tz/2023/10/26/maguire-onana-wageuka-mashujaa/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/26/maguire-onana-wageuka-mashujaa/#respond Thu, 26 Oct 2023 19:32:56 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8224 Manchester, EnglandBeki Harry Maguire na kipa Andre Onana wa Man United ambao wamekuwa wakilaumiwa kwa uchezaji wa chini ya kiwango, hatimaye wamegeuka mashujaa katika ushindi wa timu hiyo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.Onana na Maguire (pichani juu) walicheza soka la kuvutia wakati Man United ikiibuka na ushindi muhimu wa bao 1-0 katika mechi ya Ligi […]

The post Maguire, Onana wageuka mashujaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Beki Harry Maguire na kipa Andre Onana wa Man United ambao wamekuwa wakilaumiwa kwa uchezaji wa chini ya kiwango, hatimaye wamegeuka mashujaa katika ushindi wa timu hiyo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Onana na Maguire (pichani juu) walicheza soka la kuvutia wakati Man United ikiibuka na ushindi muhimu wa bao 1-0 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumanne hii dhidi ya FC Copenhagen na kuibua matumaini mapya.
Ushindi huo umekuja baada ya kocha wa Man United, Erik Ten Hag kukiri kabla ya mechi kwamba kwa mwenendo wa timu yake suluhisho pekee ni kuhakikisha wanapata ushindi ambao hatimaye ulipatikana huku Onana na Maguire waliopitia kipindi kigumu wakiwajibika ipasavyo.
Maguire alipoteza unahodha Man United huku West Ham ikimtangazia ofa ya kumsajili japo aliikataa ofa hiyo lakini zaidi ya unahodha pia alipoteza nafasi katika kikosi cha kwanza.
Kwa Onana, hivi karibuni baadhi ya mashabiki na wachambuzi walianza kuhoji ni kwa nini hasa Ten Hag alikuwa tayari kutoa kitita cha Pauni 47 milioni ili kumsajili kipa huyo kutoka Inter Milan.
Hata hivyo kuanzia mwishoni mwa wiki wachezaji hao wameanza kuibua matumaini mapya kwa kila mmoja wao kuonesha kile ambacho kimemfanya awe katika klabu hiyo.
Umahiri wa Maguire ulionekana Jumanne si tu katika kudhibiti mashambulizi bali pia ndiye mfungaji bao pekee la ushindi kwa timu yake wakati Onana aliwanyima FC Copenhagen bao la penalti ya Jordan Larsson na hivyo kupata matokeo yaliyofufua matumaini ya timu hiyo kucheza hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.
Matokeo mechi za Jumanne Ligi ya Mabingwa Ulaya
Galatasaray 1-3 Bayern Munich
Man United 1-0 FC Copenhagen
Lens 1-1 PSV Eindhoven
Sevilla 1-2 Arsenal
Union Berlin 0-1 Napoli
Sporting Braga 1-2 Real Madrid
Inter Milan 2-1 Red Bull Salzburg
Benfica 0-1 Real Sociedad

The post Maguire, Onana wageuka mashujaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/26/maguire-onana-wageuka-mashujaa/feed/ 0
Wanaomsakama Maguire wamkera Southgate https://www.greensports.co.tz/2023/09/14/wanaomsakama-maguire-wamkera-southgate/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/14/wanaomsakama-maguire-wamkera-southgate/#respond Thu, 14 Sep 2023 06:25:06 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7745 London, EnglandKocha wa England, Gareth Southgate amewajia juu wanaomsakama beki wa timu hiyo, Harry Maguire akisema hajawahi kuona mchezaji akisakamwa namna hiyo ingawa Maguire mwenyewe amesema atakabiliana na jambo hilo.Maguire (pichani) ambaye pia ni beki wa Man United alijikuta katika wakati mgumu baada ya kujifunga katika mechi ya kirafiki ya England dhidi ya Scotland, mechi […]

The post Wanaomsakama Maguire wamkera Southgate first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa England, Gareth Southgate amewajia juu wanaomsakama beki wa timu hiyo, Harry Maguire akisema hajawahi kuona mchezaji akisakamwa namna hiyo ingawa Maguire mwenyewe amesema atakabiliana na jambo hilo.
Maguire (pichani) ambaye pia ni beki wa Man United alijikuta katika wakati mgumu baada ya kujifunga katika mechi ya kirafiki ya England dhidi ya Scotland, mechi ambayo England ilishinda kwa mabao 3-1.
Hiyo ilikuwa mechi ya 59 kwa beki huyo na timu ya England lakini tangu aisaidie timu hiyo kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018 na kufikia hatua ya nusu fainali na baadaye kuifikisha katika hatua ya fainali ya Euro 2020, amekuwa na wakati mgumu katika klabu na timu ya taifa.
“Sijawahi kuona mchezaji akikumbana na kusakamwa namna hii, amekuwa mchezaji muhimu kwetu na mwenye mafanikio kwa zaidi ya miaka 10, hakika amekuwa tegemeo kwa kipindi hicho, nimekuwa nikizungumzia umuhimu wa wachezaji waandamizi, yeye ni kati yao,” alisema Southgate.
“Wakati wote anapokuwa uwanjani, utulivu ambao amekuwa akiuonesha ni wa kipekee, ni mchezaji wa hadhi ya juu na tuko naye pamoja, mashabiki wetu walikuwa wazuri kwake,” alisema Southgate.
Maguire alivuliwa unahodha katika kikosi cha Man United sababu mojawapo ikiwa ni kukosa namba ya uhakika kikosi cha kwanza lakini pia alihusishwa mno na mipango ya kuuzwa lakini ameendelea kubaki kutokana na janga la mabeki majeruhi katika timu hiyo.
Katika msimu huu wa 2023-24, Maguire amepata nafasi katika kikosi cha Man United, Sepemba 3 akingia kipindi cha pili wakati timu hiyo ikiumana na Arsenal na kulala kwa mabao 3-1.
Katika mechi na Scotland, Maguire alijifunga dakika ya 67 lakini jambo la kushangaza ni kwamba wakati akiingia kutokea benchi katika kipindi cha pili alijikuta akizomewa na mashabiki wa England jambo ambalo lilimkera Southgate.
“Kama ni mashabiki wa Scotland naweza kuelewa na wala sina cha kulalamika kwa walichokifanya lakini hayo ni matokeo ya kusakamwa kwa mchezaji huyo kwa kipindi kirefu,” alisema Southgate.

“Ni dhihaka, si mashabiki wa Scotland tu lakini hata waandishi wetu, wachambuzi wa soka au wowote wale, wametengeneza kitu ambacho sijawahi kukiona hapo kabla,” alisema Southgate.


Kwa upande wake Maguire alisema kwamba walichofanya mashabiki wa Scotland ni kama vile kuwaondolea presha wachezaji wenzake wa England na kuzielekeza kwake jambo ambalo amesema kwamba ni dogo na atakabiliana nalo.

The post Wanaomsakama Maguire wamkera Southgate first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/14/wanaomsakama-maguire-wamkera-southgate/feed/ 0
Maguire, Henderson ndani England https://www.greensports.co.tz/2023/09/01/maguire-henderson-ndani-england/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/01/maguire-henderson-ndani-england/#respond Fri, 01 Sep 2023 12:35:00 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7630 London, EnglandKocha wa timu ya Taifa ya England, Gareth Southgate ametangaza kikosi chake kwa ajili ya mechi dhidi ya Ukraine na Scotland akiwajumuisha Jordan Henderson na Harry Maguire (pichani).England itaumana na Ukraine Septemba 9 katika mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Ulaya au Euro 2024 ambayo itachezwa nchini Poland na Septemba 12 itacheza mechi ya […]

The post Maguire, Henderson ndani England first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa timu ya Taifa ya England, Gareth Southgate ametangaza kikosi chake kwa ajili ya mechi dhidi ya Ukraine na Scotland akiwajumuisha Jordan Henderson na Harry Maguire (pichani).
England itaumana na Ukraine Septemba 9 katika mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Ulaya au Euro 2024 ambayo itachezwa nchini Poland na Septemba 12 itacheza mechi ya kirafiki na Scotland.
Kiungo, Henderson, ameteuliwa baada ya kuondoka katika klabu ya Liverpool na kujiunga na Al-Ettifaq ya Saudi Arabia wakati Maguire amekuwa hana uhakika wa namba katika kikosi cha Man United na tayari amevuliwa unahodha wa timu hiyo.
Katika kikosi hicho Southgate pia amewaita kwa mara ya kwanza mshambuliaji wa Arsenal, Eddie Nketiah na beki wa kati wa Chelsea, Levi Colwill pamoja na kiungo wa Man City, Kalvin Phillips ingawa bado hajaanza kuichezea City.
Katika hatua nyingine, Southagate amemuacha katika kikosi hicho mshambuliaji wa Chelsea, Raheem Sterling akifanya hivyo kwa mara ya pili jambo ambalo linaibua hofu kuhusu majaliwa ya mchezaji huyo katika timu ya England.

“Sterling amekosekana kwa mara nyingine na ukweli ni kwamba hilo limewapa nafasi wengine kucheza vizuri na kujitengenezea mazingira katika timu, ni uteuzi mgumu na Raheem hajaufurahia lakini naamini atakuwa na msimu mzuri Chelsea, sina shaka kuhusu hilo,” alisema Southgate.


Kikosi kamili cha England na majina ya timu wanazotoka katika mabano ni kama ifuatavyo, makipa: Sam Johnstone (Crystal Palace), Jordan Pickford (Everton), Aaron Ramsdale (Arsenal)
Mabeki: Kieran Trippier (Newcastle), Kyle Walker (Man City) Ben Chilwell (Chelsea), Levi Colwill (Chelsea), Lewis Dunk (Brighton), Marc Guehi (Crystal Palace), Harry Maguire (Man United) na Fikayo Tomori (AC Milan),
Viungo: Trent Alexander-Arnold (Liverpool), Jude Bellingham (Real Madrid), Conor Gallagher (Chelsea), Jordan Henderson (Al-Ettifaq), Kalvin Phillips (Man City), Declan Rice (Arsenal)
Washambuliaji: Harry Kane (Bayern Munich), James Maddison (Tottenham), Eddie Nketiah (Arsenal), Marcus Rashford (Man United), Bukayo Saka (Arsenal), Callum Wilson (Newcastle), Eberechi Eze (Crystal Palace), Phil Foden (Man City) na Jack Grealish (Man City).

The post Maguire, Henderson ndani England first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/01/maguire-henderson-ndani-england/feed/ 0
Fernandes nahodha mpya Man United https://www.greensports.co.tz/2023/07/22/fernandes-nahodha-mpya-man-united/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/22/fernandes-nahodha-mpya-man-united/#respond Sat, 22 Jul 2023 09:35:40 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7066 Manchester, EnglandKiungo Bruno Fernandes ametangazwa kuwa nahodha mpya Man United akichukua nafasi ya Harry Maguire aliyevuliwa jukumu hilo na kocha Erik ten Hag baada ya kukosa namba ya uhakika kikosi cha kwanza.Fernandes (pichani) amekabidhiwa jukumu hilo akiwa na rekodi ya kuichezea timu hiyo mechi 185 na kufunga mabao 64 akiwa pia na asisti 54 katika […]

The post Fernandes nahodha mpya Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kiungo Bruno Fernandes ametangazwa kuwa nahodha mpya Man United akichukua nafasi ya Harry Maguire aliyevuliwa jukumu hilo na kocha Erik ten Hag baada ya kukosa namba ya uhakika kikosi cha kwanza.
Fernandes (pichani) amekabidhiwa jukumu hilo akiwa na rekodi ya kuichezea timu hiyo mechi 185 na kufunga mabao 64 akiwa pia na asisti 54 katika mashindano yote.
Kiungo huyo tayari alianza kutekeleza majukumu ya unahodha kwa muda mrefu kwenye msimu uliopita wa 2023-34 pale Maguire alipokosekana kwenye timu kwa kuwa majeruhi au kukosa namba.
Man United bado haijawa tayari kupokea ofa ya Maguire ambaye West Ham United iliwahi kumuulizia katika dirisha dogo la usajili la Januari lakini mabosi United hawakulipa umuhimu suala hilo.

“Kiungo huyu wa Ureno tayari ameshawahi kuvaa kitambaa cha unahodha cha United katika mechi kadhaa na Erik ten Hag amethibitisha kwamba sasa mchezaji huyo ataendelea na jukumu hilo moja kwa moja,” ilisema taarifa ya Man United.


Katika moja ya matukio mabaya ya kukumbukwa ya Fernandes ni siku ambayo Man United ililala mbele ya Liverpool kwa mabao 7-0 katika msimu uliopita wa 2022-23 na mchezaji huyo kulaumiwa kwa kucheza chini ya kiwango.

The post Fernandes nahodha mpya Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/22/fernandes-nahodha-mpya-man-united/feed/ 0
Ten Hag amkingia kifua Maguire https://www.greensports.co.tz/2023/04/23/ten-hag-amkingia-kifua-maguire/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/23/ten-hag-amkingia-kifua-maguire/#respond Sun, 23 Apr 2023 13:35:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5915 Manchester, EnglandKwa mara nyingine kocha wa Man United, Erik ten Hag amemkingia kifua beki na nahodha wa timu hiyo, Harry Maguire akisema ni mchezaji wa mfano kwa wachezaji wengine kwenye timu.Mara kadhaa Maguire amekuwa akibebeshwa zigo la lawama kutokana na kiwango chake cha uchezaji lakini Ten Hag ameendelea kumuamini na hajawahi kuwa tayari japo kumvua […]

The post Ten Hag amkingia kifua Maguire first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kwa mara nyingine kocha wa Man United, Erik ten Hag amemkingia kifua beki na nahodha wa timu hiyo, Harry Maguire akisema ni mchezaji wa mfano kwa wachezaji wengine kwenye timu.
Mara kadhaa Maguire amekuwa akibebeshwa zigo la lawama kutokana na kiwango chake cha uchezaji lakini Ten Hag ameendelea kumuamini na hajawahi kuwa tayari japo kumvua unahodha wa timu hiyo.
Alhamisi iliyopita, Maguire alishushiwa lawama kwa makosa aliyoyafanya katika mechi na Sevilla na kuwa sababu mojawapo ya timu hiyo kutolewa kwenye Europa Ligi.
Beki huyo anadaiwa kusababisha bao la mapema la Sevilla huku kiwango chake kikiwa mjadala kwa mara nyingine baada ya Man United kulala kwa mabao 3-0 na hivyo kutolewa katika michuano hiyo kwa jumla ya mabao 5-2.
Ten Hag hata hivyo anaonekana kuwa tofauti akisema kwamba Maguire mwenye umri wa miaka 30 anaendelea kuwa mtu muhimu kwenye kikosi chake.

“Maguire ana jukumu muhimu kwenye timu, ndiye nahodha, anaongoza wenzake, anawasiliana na kocha anaishawishi timu, ni mchezaji wa mfano katika mazoezi,” alisema Ten Hag.


Maguire si mchezaji pekee aliyeshushiwa lawama baada ya matokeo mabaya dhidi ya Sevilla, hali ambayo pia iliibua hoja ya uwezekano wa wachezaji walio wengi kuachwa baada ya msimu ingawa Ten Hag amesema anaangalia hali ya sasa katika kikosi chake.
“Nafikiria kuhusu kuiboresha timu hii na wachezaji hawa hawa, hiyo ndiyo kazi yangu na jopo la makocha na wachezaji, fikra zetu zote zipo katika mchakato huo na si mchakato mwingine ambao utatutoa kwenye mstari,” alisema.
“Najua kundi hili la wachezaji linaweza kufanya vizuri, wamethibitisha hilo mara nyingi katika msimu huu, tumepiga hatua kubwa katika msimu huu japo ni kweli kuna hatua za kuchukua, tuna mechi nyingi za kucheza na tunatakiwa kuthibitisha ubora,” aliongeza.
Man United, leo Jumapili ina mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Brighton & Hove Albion kwenye dimba la Wembley na Ten Hag amesema kwamba timu yake inatakiwa kuwa na mtazamo imara na kujifunza kutorudia makosa yaliyowakwanza katika mechi zao.

The post Ten Hag amkingia kifua Maguire first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/23/ten-hag-amkingia-kifua-maguire/feed/ 0
Ten Hag amhofia Rashford, amfurahia Maguire https://www.greensports.co.tz/2023/04/09/ten-hag-amhofia-rashford-amfurahia-maguire/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/09/ten-hag-amhofia-rashford-amfurahia-maguire/#respond Sun, 09 Apr 2023 19:22:57 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5745 Manchester, EnglandKocha wa Man United, Eric ten Hag amesema mambo si mazuri kwa straika wake, Marcus Rashford ingawa amefurahia kiwango cha beki Harry Maguire ambaye kwa muda mrefu amekuwa akisugua benchi.Rashford aliumia jana Jumamosi wakati timu hiyo ikiichapa Everton mabao 2-0 katika mechi ambayo Ten Hag pia alimpa nafasi nahodha na beki wa kati Maguire […]

The post Ten Hag amhofia Rashford, amfurahia Maguire first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kocha wa Man United, Eric ten Hag amesema mambo si mazuri kwa straika wake, Marcus Rashford ingawa amefurahia kiwango cha beki Harry Maguire ambaye kwa muda mrefu amekuwa akisugua benchi.
Rashford aliumia jana Jumamosi wakati timu hiyo ikiichapa Everton mabao 2-0 katika mechi ambayo Ten Hag pia alimpa nafasi nahodha na beki wa kati Maguire ambaye amepoteza namba kikosi cha kwanza.
Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu England (EPL), Rashford alipata matatizo ya misuli muda mfupi kabla ya filimbi ya kumaliza mchezo huo kupulizwa na baadaye alionekana akitoka uwanjani katika hali ya unyonge.
Na ingawa Ten Hag awali alipoulizwa kuhusu mchezaji huyo na ukubwa wa maumivu aliyoyapata alikataa kuzungumzia hilo kwa undani na kuhoji wenye hofu hiyo kama wao ni madaktari.
Kocha huyo hata hivyo alilalamikia ugumu wa ratiba inayoikabili timu hiyo na kusema kuwa mambo si mazuri kwa mchezaji huyo na kuhusisha ratiba hiyo ngumu na maumivu ya mchezaji huyo.

“Tunalazimika kusubiri hali haionekani kuwa nzuri, hali hii inaweza kuepukwa, sayansi na tafiti zote zinasema wachezaji wanahitaji muda kwa ajili ya kupumzika na kujiweka sawa,” alisema Ten Hag.


“Hii inachangiwa na ratiba tuliyonayo hadi tunajikuta katika mazingira ya aina hii na sasa tunachoweza kufanya ni kuomba asiwe wa kutolewa kwenye kikosi moja kwa moja,” alisema.
Ten Hag pia alikiri kwamba angeweza kumtoa Rashford baada ya United kupata bao la pili dakika ya 19 lakini hakuwa tayari kufanya hivyo kwa sababu alitaka mfungaji wake huyo bora apate muda wa kucheza pamoja na Anthony Martial aliyerejea.
“Sidhani kama kuna kocha yeyote katika kipindi hiki cha msimu anaweza kubadili badili wachezaji wake kwa sana, nilikuwa na fikra hizo za kumtoa nje lakini kwa kipindi hiki ndio kwanza Anthony Martial amerejea unataka wawe pamoja,” alisema.
“Wanapokuwa pamoja hapo tunakuwa na wafungaji wawili ambao wanaweza kumaliza mechi kitu ambacho tunakihitaji katika hatua hizi za mwisho za msimu ili kuwa na mafanikio,” aliongeza Ten Hag.
Kuhusu Maguire, Ten Hag pia alieleza kufurahishwa na kiwango cha nahodha huyo akisema kwamba hapo kabla hakumuona akicheza kwa ubora huo.
“Huyu alikuwa Harry Maguire mwingine kabisa, tofauti na yule wa wiki au miezi ya mwanzo, mambo hayakuwa rahisi kwake lakini ni yeye aliyekuwa akitaka kucheza na alicheza vizuri mno leo (jana) awe na mpira au asiwe na mpira, aliwadhibiti wapinzani wake, aliongoza mchezo na kutoa pasi,” alisema Ten Hag.
Maguire beki aliyesajiliwa kwa Pauni 80 milioni amekuwa na wakati mgumu kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Man United kwa kilichoonekana kuwa ni kushuka kiwango lakini Ten Hag ameendelea kumuamini katika nafasi ya nahodha wa timu.

The post Ten Hag amhofia Rashford, amfurahia Maguire first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/09/ten-hag-amhofia-rashford-amfurahia-maguire/feed/ 0